Feb 24, 2024 10:44 UTC
  • Mamilioni ya Wayemen waandamana katika mshikamano na Wapalestina wanaodhulumiwa Gaza

Mamilioni ya Wayemeni wameandamana kote katika nchi yao kuonyesha uungaji mkono kwa Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, ambao wanakabiliwa na vita vya mauaji ya kimbari vya utawala dhalimu wa Israel.

Mikutano hiyo ilifanyika katika majimbo mbalimbali kote Yemen siku ya Ijumaa. Kwa mujibu wa mtandao wa televisheni wa al-Masirah wa Yemen, "Washiriki walithibitisha uthabiti na azma katika msimamo wao wa kutetea harakati ya kuikomboa ardhi ya Palestina ambayo inakaliwa kwa mabavu na kukoloniwa na utawla haramu wa Israel.

Wananchi wa Yemen wamekuwa wakifanya maandamano kama hayo kila Ijumaa tangu tarehe 7 Oktoba 2023, wakati utawala huo ulipoanzisha vita dhidi ya Gaza kwa himaya ya Marekani.

Utawala huo kwa wakati mmoja umekuwa ukitumia mzingiro wa kila upande dhidi ya mwambao wa pwani, kuzuia mtiririko wa maji, chakula, umeme, na vifaa vya matibabu katika eneo hilo.

Mauaji Gaza

Katika kipindi cha takribani miezi mitano, Israel imewau Wapalestina wasiopungua  29,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na kujeruhi makumi ya maelfu ya wengine.

Ijumaa hii, maandamano ambayo yalifanyika kote Yemen kutangaza mshikamano na watu wa Gaza  kote Yemen, yalishuhudia idadi kubwa ya washiriki ikilinganishwa na yale ya wiki zilizopita.

Waandamanaji walioshiriki maandamano hayo yaliyofanyika katika mji mkuu wa Yemen wa Sana'a walitoa taarifa "kulaani jinai zinazoendelea za Wazayuni." Aidha walikaani  kimwa cha kimataifa na  kile walichokiita, "misimamo dhaifu ya Waarabu kuhusu ukatili wa Isarel."

Taarifa hiyo pia imepongeza oparesheni ambazo jeshi la Yemen limekuwa likizifanya dhidi ya meli za Israel na zile zinazoelekea katika bandari za ardhi zinazokaliwa kwa mabavu kama njia ya kuzidisha mashinikizo dhidi ya utawala wa Israel na waungaji mkono wake.

Wananchi wa Yemen waliapa kwamba operesheni hizo zitaendelea "hadi vita vitakapomalizika na mzingiro wa Gaza kuondolewa."