Mar 02, 2024 11:49 UTC
  • Israel yapuuza malalamiko ya dunia, yaendelea kumwaga damu za Wapalestina

Kwa akali Wapalestina 17 wameuawa shahidi katika mashambulizi mapya ya anga ya utawala wa Kizayuni wa Israel yaliyolenga nyumba tatu za Wapalestina katika maeneo ya Deir el-Balah na Jabalia katika Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa kanali ya talevisheni ya al-Jazeera, wanajeshi wa Israel waliwauwa shahidi makumi ya watu waliokuwa katika umati uliokuwa ukisubiri kupatiwa misaada ya kibinadamu huko kusini mwa Gaza katika hujuma hizo za anga usiku wa kuamkia jana. 

Mkurugenzi wa Hospitali ya al-Awda amesema asilimia 80 ya majeruhi wa mashambulizi hayo waliopelekewa hospitalini hapo wana majeraha ya risasi. 

Habari zaidi zinasema kuwa, watu wengine watatu wameaga dunia kutokana na majeraha ya risasi na hivyo kufanya idadi ya waliopoteza maisha katika hujuma mpya za Wazayuni kuongezeka na kufikia watu 115.

Timu ya Umoja wa Mataifa imesema aghalabu ya waliojeruhiwa kwenye hujuma hizo za Israel huko kusini mwa Gaza walikuwa na majeraha ya risasi. 

Aidha kwa mujibu wa Brigedi za Izzuddin al-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS, mateka saba wa Israel wameaga dunia kutokana na mashambulio hayo ya Israel.

Wanajeshi makatili wa Kizayuni 

Viongozi wa makanisa ya al-Quds wamelaani jinai hizo za kutisha za Wazayuni, huku la shirika la Amnesty International likitoa wito wa kufanyika uchunguzi wa haraka kuhusu mauaji hayo makubwa ya Wapalestina yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina waliokuwa wakisubiri kupokea misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza.

Wakati walimwengu wakilaani jinai hiyo ya kinyama, Waziri wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel mwenye misimamo mikali ya chuki, Itamar Ben-Gvir amewapongeza wanajeshi wa utawala huo walioua zaidi ya Wapalestina 115 waliokuwa wakisubiri misaada ya kibinadamu.

Tags