Hamas: Asilimia 70 ya mateka wa Kizayuni wameuawa katika mashambulizi ya Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i111878
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetangaza kuwa mashambulizi ya utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza, ambao unakabiliwa na vita vya mauaji ya kimbari ya utawala huo, yameuwa asilimia 70 ya mateka wa Kizayuni, ambao walikuwa wakishikiliwa na harakati hiyo ya muqawama tangu baada ya operesheni ya Kimbunga cha Al Aqsa mwezi Oktoba mwaka jana.
(last modified 2024-05-18T04:00:03+00:00 )
May 18, 2024 04:00 UTC
  • Hamas: Asilimia 70 ya mateka wa Kizayuni wameuawa katika mashambulizi ya Israel

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetangaza kuwa mashambulizi ya utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza, ambao unakabiliwa na vita vya mauaji ya kimbari ya utawala huo, yameuwa asilimia 70 ya mateka wa Kizayuni, ambao walikuwa wakishikiliwa na harakati hiyo ya muqawama tangu baada ya operesheni ya Kimbunga cha Al Aqsa mwezi Oktoba mwaka jana.

Khalil al Hayya Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas ametangaza taarifa hiyo katika mahojiano yake na televisheni ya al Manar ya Lebanon. Amesema, adui Mzayuni anataka kuwakomboa kwa nguvu mateka wake waliosalia kupitia mashambulizi ya anga. Waisraeli wasiopungua 250 walitekwa nyara Oktoba 7 mwaka jana katika oparesheni  ya kulipiza kisasi iliyotekelezwa na makundi ya mapambano ya ukombozi ya Palestina huko Gaza. 

Mateka wa utawala wa Kizayuni 

Wakati huo huo Wapalestina wasiopungua 35,272 wameuawa shahidi katika vita vya mauaji ya kimbari ya Israel yaliyofuatia oparesheni ya Kimbunga cha al Aqsa. 

Harakati ya Hamas iliwaachia huru mateka 105 wa utawala wa Kizayuni katika mapatano ya kusimamisha vita ya wiki moja kati ya pande mbili mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana.

Hivi karibuni harakati hiyo ya mapambano ya Palestina ilikubali pendekezo jingine la kusitisha vita, hata hivyo utawala wa Kizayuni umekataa pendekezo hilo. 

Katika mahojiano hayo na televisheni ya Lebanon ya al Manar, Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas amesema: "Pendekezo la kusimamisha mapigano lililowasilishwa kwetu lilikurubiana sana na matwaka yetu, lakini adui hakuheshimu pendekezo hilo wala wapatanishi.”

Al Hayya Al-Hayya ametilia mkazo suala la kutekelezwa matakwa yao akisema kuwa makubaliano yoyote yatakayofikiwa yanapaswa kuamuru kusitishwa kikamilifu mashambulizi na mauaji ya kimbari ya Israel, kuondoka wanajeshi wote wa Israel huko Gaza, na kisha kufikiwa mapatano ya kubadilishana mateka kati ya pande mbili .