Dec 02, 2022 08:01 UTC

Katika hali ambayo serikali ya Morocco imetangaza uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel, wananchi wa nchi hiyo ya Kiarabu na ya Waislamu, wamezidi kuonesha kutokubaliana na uamuzii huo wa utawala wa kifalme wa Morocco.

Baada ya kufanikiiwa kupanda kwenye awamu ya mtoano ya mashindano ya Kombe la Dunia la Kandanda 2022 yanayoendelea huko Qatar,  Timu ya Taifa ya Morocco imesheherehekea ushindi huo kwa kupeperusha juu pia bendera ya Palestina.

Timu ya Morocco imeingia kwenye hatua ya mtoano ya mashindano hayo baada ya kuichabanga Canada mabao 2-1. Hii ni mara ya pili kwa Timu ya Taifa ya Morocco kuingia hatua hiyo ya mtoano tangu mwaka 1986.

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Morocco wamesujudu kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwapa ushindi huo na vile vile wamepeperusha bendera za Morocco na Palestina kwa pamoja, katika kusherehekea ushindi huo.

Mashindano ya Kombe la Dunia 2022 huko Qatar yameitangaza vizuri kadhia ya Palestina na kuonesha ni kiasi gani walimwengu wanachukizwa na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel. Mara kwa mara Waislamu na wapenda haki wameonekana wakibeba na kupeperusha juu bendera ya Palestina ili kutangaza uungaji mkono wao kwa taifa hilo linalodhulumiwa kila upande na kwa makumi ya miaka sasa.

Mchezaji wa timu ya taifa ya Morocco, Jawad El Yamiq kama anavyoonekana hapa chini akiwa anasherehekea ushindi huo akiwa amebeba bendera ya Palestina.

 

Tags