Jan 30, 2023 02:46 UTC
  • Pigo kali la Wapalestina kwa baraza lenye misimamo mikali la Israel

Siku moja tu baada ya kutekelezwa jinai ya Wazayuni dhidi ya Wapalestina huko Jenin, kijana mmoja wa Kipalestina ametekeleza oparesheni ya kishujaa katika mji mtakatifu wa Quds inayokaliwa kwa mabavu na kusababisha vifo vya Wazayuni 10.

Alkhamisi asubuhi na kwa msaada wa moja kwa moja wa shirika la usalama wa ndani la utawala ghasibu wa Israel Shabak, askari kandamizi wa utawala huo haramu walishambulia kambi ya wakimbizi huko Jenin, ambapo Wapalestina 11 waliuawa na wengine 20 wakajeruhiwa. Baada ya jinai hiyo, viongozi wa mapambano ya Palestina walitangaza kuwa, Wazayuni watalipa gharama kubwa kutokana na jinai hiyo. Ziyad al-Nakhleh, Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina amesema kuwa, licha ya jinai zote hizo zinazotekelezwa dhidi Wapalestina wasio na hatia, lakini wapiganaji shupavu na shujaa wa Palestina wataendelea kubaki katika uwanja wa mapambano dhidi ya adui. Siku moja baadaye, yaani siku ya Ijumaa, shahidi Khairy Alqam, kijana wa Kipalestina mwenye umri wa miaka 21, alitekeleza operesheni ya kishujaa katika kitongoji cha Wazayuni cha Nabii Yaqoub huko Quds inayokaliwa kwa mabavu, ambayo ilisababisha vifo vya Wazayuni 11 na kupelekea wengine kadhaa kujeruhiwa. Kwa hiyo, operesheni ya Shahidi Khairy Alqam ilikuwa utekelezaji wa onyo lililotolewa na harakati ya mapambano ya Palestina kufuatia jinai ya Jenin.

Benjamin Netanyahu

Nukta nyingine muhimu ni kwamba oparesheni ya Shahidi Khairy Alqam ni pigo kubwa zaidi ambalo limetolewa na Wapalestina dhidi ya Wazayuni katika kipindi cha miongo miwili iliyopita. Kwa upande mmoja, operesheni hiyo imefanyika katika hali ambayo viongozi na maafisa usalama vya Israeli wamechukua hatua kali zaidi za kiusalama katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, na kwa upande mwingine, imeua Wazayuni 11 jambo ambalo lilikuwa halijawahi kutokea mjini Quds katika miaka 20 iliyopita. Ukali wa operesheni hiyo umempelekea Waziri wa Vita wa Israel, ambaye alikuwa amesafiri kwenda Marekani, kurejea nyumbani, na Netanyahu na Ben Gvir, Waziri wa Usalama wa Ndani wa utawala huo, pia kulazimika kutembelea binafsi eneo la operesheni.

Jambo jingine ni kwamba operesheni hiyo imekuwa jibu madhubuti na la mapema kwa baraza lenye misimamo mikali la Benjamin Netanyahu ambalo liliundwa mwezi mmoja uliopita. Katika kipindi hiki, hususan, Itamar Bin Gvir, Waziri wa Usalama wa Ndani, ameonyesha hadharani mienendo na sera kali za kibaguzi dhidi ya Wapalestina, kwa namna ambayo Wapalestina 30 wameuawa shahidi. Operesheni ya Shahidi Khairy Alqam imetoa pigo zito na kubwa kwa baraza la mawaziri la Netanyahu kadiri kwamba waziri mkuu huyo wa utawala wa Kizayuni amekiri hadharani kuhusu mafanikio ya operesheni hiyo ya Quds kwa kusema: "Tumeshuhudia shambulio baya zaidi katika miaka ya hivi karibuni."

Nukta nyingine ya kistratijia ni kwamba operesheni hiyo imetekelezwa na Mpalestina mwenye umri wa miaka 21 pekee. Hili linaonyesha kuwa moyo wa mapambano na kutoogopa vitisho vya adui Mzayuni umeimarika miongoni mwa kizazi cha vijana wa Kipalestina, na jambo hilo limeibua hofu na mkanganyiko mkubwa katika baraza la mawaziri la Israel. Hofu imekuwa kubwa kiasi kwamba walowezi kadhaa wamemuhusisha Ben Gvir mwenyewe na operesheni za kulipiza kisasi zinazofanywa na wanamapambano wa Palestina. Kuhusiana na hilo Hizbullah ya Lebanon imetaja operesheni iliyotokelezwa huko Quds inayokaliwa kwa mabavu kuwa ni operesheni ya kishujaa na kuongeza kuwa imewatikisa Wazayuni na kuwatia hofu na wasiwasi mkubwa.

Itamar Bin Gvir

Suala jingine muhimu ni radiamali iliyotolewa na Uturuki, Imarati na Saudi Arabia katika uwanja huo. Nchi tatu hizo zimelaani operesheni hiyo iliyotekelezwa Ijumaa usiku huko Quds bila kuzungumzia jinai iliyofanywa na Wazayuni dhidi ya raia wa kawaida katika kambi ya wakimbizi huko Jenin. Msimamo wa nchi hizo kuhusu tukio hilo kwa mara nyingine unathibitisha wazi kwamba Wapalestina hawapaswi kutegemea uungaji mkono wa nchi vibaraka na zinazofanya mapatano na maadui wa Uislamu ili kujilinda, bali wanapaswa kuendeleza msingi muhimu wa "kujisaidia mwenyewe kwanza" kabla ya kusaidiwa na jirani. Kwa mujibu wa msingi huo, kila nchi ina haki ya kujilinda yenyewe dhidi ya vitisho na maadui wa kigeni.

Tags