Pezeshkian asisitiza himaya ya pande zote ya Iran kwa Palestina na kukombolewa Quds
https://parstoday.ir/sw/news/religion-i113946-pezeshkian_asisitiza_himaya_ya_pande_zote_ya_iran_kwa_palestina_na_kukombolewa_quds
Rais mteule wa Iran amesisitiza himaya na uungaji mkono wa pande zote wa Jamhuri ya Kiislamu kwa kadhia ya Palestina na kukombolewa Quds inayokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.
(last modified 2024-07-11T09:54:46+00:00 )
Jul 11, 2024 09:54 UTC
  • Pezeshkian asisitiza himaya ya pande zote ya Iran kwa Palestina na kukombolewa Quds

Rais mteule wa Iran amesisitiza himaya na uungaji mkono wa pande zote wa Jamhuri ya Kiislamu kwa kadhia ya Palestina na kukombolewa Quds inayokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.

Dkt. Masoud Pezeshkian ambaye anatarajiwa kuapishwa mwishoni mwa mwezi huu amesema hayo katika risala yake kwa Ismail Hania, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ambapo sambamba na kushukuru salamu za pongezi za mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas, rais huyo mteule amesisitiza kuendelea uungaji mkono wa pande zote wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa taifa madhulumu la Palestina hadi kufikiwa malengo yote matukufu, taifa hilo kupata haki zake na vilevile kukombolewa Quds Tukufu.

 

Sehemu moja ya risala yake hiyo inasema, kwa kuzingatia misingi na malengo matukufu ya Mapinduzi ya Kiislamu na ndani ya mfumo wa fikra za Imam Khomeini (RA) na miongozo ya Kiongozi Muadhamu, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaona kuwa ni wajibu wake wa kibinadamu na Kiislamu. kuliunga mkono taifa la Palestina na mapambano yake dhidi ya kukaliwa kwa mabavu na ubaguzi wa rangi wa utawala wa Kizayuni.

Aidha Rais mteule wa Iran amesema: Nina hakika kwamba katika kivuli cha kusimama kidete kwa kihistoria kwa taifa la muqawama la Palestina na Gaza inayodhulumiwa na yenye nguvu na mapambano ya kishujaa ya wapiganaji wa muqawama wa Palestina katika vita vya hivi sasa, ushindi na nusra ya Mwenyezi Mungu vitapatiwa taifa la Palestina.