Jan 05, 2024 12:21 UTC
  • Israel yaendeleza mashambulizi yake ya anga na mizinga Ukanda wa Gaza leo Ijumaa

Ndege za kivita na mizinga ya utawala wa Kizayuni kwa mare nyingine tena leo Ijumaa zimeyashambulia maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza.

Shirika la habari la Palestina al Yaum limeripoti kuwa maeneo ya katikati ya Ukanda wa Gaza yameshuhudia miripuko mikubwa huku wanajeshi vamizi wa utawala wa Kizayuni wakiushambulia mnara wa al Farooq katika kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ya Al Nusirat katikati ya Gaza.  

Huko kusini mwa Ukanda wa Gaza pia wanajeshi wa utawala ghasibu wa Kizayuni wameyashambulia kwa mizingia maeneo mbalimbali ya mji wa Khan Yunis. Katika hujuma hiyo, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wameishambulia nyumba moja katika eneo la al Qararah kusini kwa Gaza na kuwauwa shahidi Wapalestian watatu na kujeruhi watano. 

Mauaji ya kimbari ya Israel Gaza 

Aidha ndege za kivita za utawala haramu wa Israel zimeipiga kwa mabomu nyumba moja katika mji wa Rafah kusini wa Gaza na kuwaua shahidi Wapalestina watano. Wanajeshi wa utawala wa Israel leo asubuhi pia wameushambulia mji wa al Khalil na kukabiliana na vijana wa Kipalestina. 

Raia katika nchi mbalimbali katika eneo na duniani kwa ujumla wameendelea kulaani vikali mashambulizi ya jeshi la utawala wa Kizayuni huko Ukanda wa Gaza hata hivyo hadi sasa taasisi za kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa zimeshindwa kusitisha mashambulizi hayo dhidi ya wakazi wa ukanda huo. 

Tags