Kocha mwanamke wa Futsal Iran aingia katika orodha ya makocha kumi bora duniani
Kocha mwanamke wa timu ya Futsali ya Saipa Iran ameng'ara na kuuingia katika orodha ya makocha kumi bora duniani katika chezo wa Futsal.
Tovuti ya Futsal Planet imechapisha majina ya makocha 10 bora wa timu za vilabu kwa mwaka uliomalizika hivi karibuni wa 2024, na jina la Fatemeh Sharif, mkufunzi wa zamani wa timu ya taifa ya wanawake ya Iran ya futsali na kocha mkuu wa timu ya Saipa linaonekana katika orodha hiyo.
Tovuti hiyo kila mwaka hutoa orodha na makocha, wachezaji na timu bora kwa upande wa wanawake katika mchezo wa futsal.
Fatemeh Sharif amekuwa kocha mkuu wa timu ya futsal ya wanawake ya Saipa ya Iran tanguu mwanzoni mwa mwaka jana na ameweza kupata matokeo mazuri akiwa na timu hii. Kwa sasa Saipa iko katika nafasi ya pili kwenye jedwali la Ligi Kuu ya Wanawake ya Futsal ya Iran kwa mchezo mmoja pungufu kwa Naft Abadan. Hata hivyo, zimesalia mechi tano zaidi hadi mwisho wa msimu huu na inabakia kuonekana ni timu gani itashinda Ligi Kuu ya Futsal ya Wanawake.