Upotoshaji mkubwa! Al Jazeera yaficha shukrani za msemaji wa Hamas kwa Iran
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i121708-upotoshaji_mkubwa!_al_jazeera_yaficha_shukrani_za_msemaji_wa_hamas_kwa_iran
Kitengo cha "habari za punde" cha televisheni ya Al Jazeera ya Qatar kwenye mitandao ya kijamii, katika hatua ya kushangaza, kimechuja shukrani zilizotolewa na Obaida, msemaji wa "Brigedi za Izzuddin al-Qassam," tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) kwa Iran na Yemen.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Jan 21, 2025 03:47 UTC
  • Upotoshaji mkubwa! Al Jazeera yaficha shukrani za msemaji wa Hamas kwa Iran

Kitengo cha "habari za punde" cha televisheni ya Al Jazeera ya Qatar kwenye mitandao ya kijamii, katika hatua ya kushangaza, kimechuja shukrani zilizotolewa na Obaida, msemaji wa "Brigedi za Izzuddin al-Qassam," tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) kwa Iran na Yemen.

"Sehemu ya habari za hivi punde" ya televisheni ya Al Jazeera kwenye mitandao ya kijamii imeficha na kuchuja shukrani za Abu Obaida, msemaji wa tawi la kijeshi la Hamas, kwa Iran na Yemen, na badala yake kutuma tu ujumbe wa shukrani wa maandishi kwa Qatar na Jordan.

Katika hotuba yake juzi Jumapili usiku, Abu Obaida aliishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Yemen kwa misaada na uungaji mkono wao kwa Muqawama na wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina.

Msemaji wa tawi la kijeshi la Hamas alisema: "Napenda kutoa salamu na ashukrani za dhati kwa wale wote walioshirikiana na watu wa Gaza katika kukabiliana na dhulma na ueneviu na kushirikiana nasi katika Operesheni ya Kimbunga cha al Aqsa. Nawashukuru hasa ndugu zetu wakweli, Ansarullah, na taifa ndugu, katika Yemen yenye hikima na imani. Tunawapongeza ndugu na wenzetu katika mapambano ya silaha, Muqawama wa Kiislamu huko Lebanon (Hizbullah). Vilevile tunawashukuru ndugu zetu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa msaada wao wa daima na endelevu na kushiriki kwao katika mapambano haya ya kihistoria kupitia Operesheni za Ahadi ya Kweli na uungaji mkono wao unaoendelea kwa njia zote. Tunawashukuru pia ndugu zetu huru katika Muqawama wa kishujaa huko Iraq..

Kuchuja sehemu hii ya kauli muhimu za Abu Obaida kwenye chombo cha habari kama Al Jazeera ni jambo la ajabu na kielelezo cha kuficha ukweli.

Televisheni ya Al Jazeera ya Qatar iliheshimiwa kwa utangazaji wake wa kina wa habari za Gaza; Hata hivyo, mapungufu haya na uchujaji wa ajabu katika utoaji wa habari, na vilevile uungaji mkono wa chombo hicho cha habari kwa makundi ya kigaidi yenye silaha kama vile Tahrir al-Sham huko Syria, ambayo yanapingana na Mhimili wa Muqawama na kufanya kazi kwa maslahi ya Wazayuni, kunaweza kutoa pigo zito na kubwa kwa uaminifu wa chombo hicho  miongoni mwa mataifa ya eneo la Asia Magharibi.