Wanajeshi wa Israel wamuua mwanamke mjamzito wa Kipalestina na kichanga chake katika Ukingo wa Magharibi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i122534-wanajeshi_wa_israel_wamuua_mwanamke_mjamzito_wa_kipalestina_na_kichanga_chake_katika_ukingo_wa_magharibi
Wanajeshi wa Israel wamemuua kwa kumpiga risasi mwanamke Mpalestina aliyekuwa na ujauzito wa miezi minane na kichanga kilichokuwa tumboni mwake wakati askari jeshi wa utawala huo ghasibu walipovamia kambi ya wakimbizi ya Nur Shams kaskazini magharibi mwa Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
(last modified 2026-05-20T03:07:53+00:00 )
Feb 09, 2025 23:13 UTC
  • Wanajeshi wa Israel wamuua mwanamke mjamzito wa Kipalestina na kichanga chake katika Ukingo wa Magharibi

Wanajeshi wa Israel wamemuua kwa kumpiga risasi mwanamke Mpalestina aliyekuwa na ujauzito wa miezi minane na kichanga kilichokuwa tumboni mwake wakati askari jeshi wa utawala huo ghasibu walipovamia kambi ya wakimbizi ya Nur Shams kaskazini magharibi mwa Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.

Wizara ya Afya ya Palestina jana ilitoa taarifa na kusema imemtambua mhanga wa uvamizi wa jana wa jeshi la Israel huko Nur Shams kuwa ni Sundus Jamal Shalabi aliyekuwa na umri wa miaka 23 na kichanga chake wakati wanajeshi wa Israel walipomfyatulia risasi ambayo pia ilimjeruhi mume wake. 

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina, timu za matibabu hazikuweza kuokoa maisha ya kichanga hicho kwa sababu wanajeshi wa Israel waliotekeleza mauaji hayo walizuia kupelekwa majeruhi hospitali.

Mama huyo mjamzito ameuwa shahidi wakati alipokuwa akijaribu kuondoka katika makazi yao akiwa pamoja na mumewe huko Nur Shams na kuelekea katika maeneo salama ili kuhepa mashambulizi ya wanajeshi wa utawala wa Israel huko katika Ukingo wa Magharibi. 

Mapema jana Jumapili wanajeshi wa utawala wa Israel walifika katika kambi ya wakimbizi wa Palestina ya Nur Shams wakiwa na silaha nzito na mabuldoza na kuanza kuvamia makumi ya makazi ya Wapalestina.