Hali si hali, mamia ya wanajeshi wa Israel wakamatwa wakitoroka jeshini
(last modified Tue, 06 May 2025 11:01:07 GMT )
May 06, 2025 11:01 UTC
  • Hali si hali, mamia ya wanajeshi wa Israel wakamatwa wakitoroka jeshini

Wakati jeshi la utawala wa Kizayuni likikaribia kusambaratika kutokaana na uhaba wa wafanyakazi, wimbi la wanajeshi wa Israel wanaokwepa kuhudumu jeshini nalo linazidi kuongezeka hususan kutokana na hofu ya kutumwa kwenye kinamasi cha Ghaza.

Shirika la Habari la Fars limenukuu taarifa ya Kanali ya 7 ya Televisheni ya Israel ikifichua leo Jumanne kwamba tangu mwanzoni mwa mwaka huu, wanajeshi 340 wa Israel wamekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion wakitoroka na kuelekea nje ya ardhi za Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, 70 kati ya wanajeshi wa Israel waliotiwa mbaroni, walijaribu kutoroka walipokuwa wakihudumu katika jeshi la Israel, na wengi wao walikuwa ni kutoka kwenye harakati ya Waorthodoksi maarufu kwa jina la "Haredi."

Duru hizo za Israel hazikufichua utambulisho wa wafungwa wengine; lakini zimeeleza kuwa jeshi la Israel linapanga kutekeleza mpango uitwao "Mercy for Deserters from Service" kwa muda wa wiki moja ili kuhakikisha wanajeshi wote waliotoroka wanajea jeshini au anapewa adhabu kali jela.

Duru hizo zimeripoti kuwa mpango huo kwa sasa unajadiliwa kati ya maafisa wa jeshi wa jeshi na unatarajiwa kuanza kutekelezwa karibuni hivi.

Baada ya kuzuka vita katika Ukanda wa Ghaza Oktoba 7, 2023, jeshi la Israel limekumbwa na changamoto kubwa ya uhaba wa wafanyakazi na ongezeko la wanajeshi wanaotoroka.

Kuitwa jeshini vikosi vya akiba ili vishiriki katika vita vya Ghaza kumeweka shinikizo kubwa mno kwa jeshi la utawala huo katili na kusababisha wanajeshi wengi kuasi na kutoridhishwa na utendaji wa serikali.

Taarifa zinasema kuwa, idadi kubwa ya askari wa akiba wamekataa kuripoti kazini na wanatafuta njia za kukimbia vitani kutokana na muda mrefu wa kuhudumu jeshini, uchovu vitani wasiwasi wa kiuchumi na kukosa mustakbali mzuri.