Ben-Gvir awaruhusu walowezi wa Kizayuni kuimba na kudansi kwenye Msikiti wa Al-Aqsa
Waziri maluuni wa mambo ya ndani wa utawala wa Kizayuni wa Israel Itamar Ben-Gvir ametoa ruhusa kwa walowezi haramu wa Kizayuni kuimba na kudansi kwenye eneo la Msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa Baitul-Muqaddas unaokaliwa kwa mabavu.
Chaneli ya 7 ya televisheni ya Israel imesema: “kwa mara ya kwanza katika miaka kadhaa, wageni wa Kiyahudi wameruhusiwa kuimba na kudansi hadharani katika eneo takatifu, kulingana na sera mpya iliyoanzishwa na Ben-Gvir”.
Ben-Gvir, ambaye yeye mwenyewe ni mlowezi anayeongoza chama cha mrengo wa kulia chenye misimamo mikali ya chuki cha Nguvu ya Kiyahudi, ndiye anayesimamia pia jeshi la polisi la Israel.
Hatua ya waziri huyo wa kizayuni inaakisi mabadiliko yanayokinzana na kanuni na taratibu za huko nyuma zinazohusu eneo takatifu la Msikiti wa Al-Aqsa.
Kwa mujibu wa chaneli ya 7 ya televisheni ya utawala wa Kizayuni, polisi ya utawala huo sasa imetakiwa iruhusu kufanyika ibada na kuimbwa nyimbo za kiyahudi na kizayuni katika eneo lote la uwanja wa Misikiti mtukufu wa Al-Aqsa. Imeelezwa kuwa kamishna wa polisi Kobi Shabtai amefikisha amri hiyo kwa maafisa wa jeshi hilo.
Wiki tatu nyuma, iliripotiwa kuwa, Ben-Gvir alikutana ofisini kwake na viongozi wa makundi ya walowezi wa Kizayuni wanaoshupalia wazayuni kupatiwa fursa ya kujifaragua katika uwanja wa Msikiti wa Al-Aqsa, kibla cha kwanza cha Waislamu na Msikiti wa tatu wenye utukufu mkubwa zaidi katika Uislamu…/