Mji wa Bat Yam umekuwa kama Gaza baada ya mashambulizi ya makombora ya Iran dhidi ya Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i127788-mji_wa_bat_yam_umekuwa_kama_gaza_baada_ya_mashambulizi_ya_makombora_ya_iran_dhidi_ya_israel
Gazeti la Israel la lugha ya Kiibrania limeripoti kuwa mji wa Bat Yam katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) sasa unafanana na maeneo yaliyoathiriwa na vita ya Ukanda wa Gaza baada ya mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran dhidi ya utawala wa Israel.
(last modified 2025-06-30T07:57:40+00:00 )
Jun 30, 2025 07:57 UTC
  • Mji wa Bat Yam umekuwa kama Gaza baada ya mashambulizi ya makombora ya Iran dhidi ya Israel

Gazeti la Israel la lugha ya Kiibrania limeripoti kuwa mji wa Bat Yam katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) sasa unafanana na maeneo yaliyoathiriwa na vita ya Ukanda wa Gaza baada ya mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran dhidi ya utawala wa Israel.

Gazeti la Calcalist limeripoti kuwa, kwa mujibu wa data mpya, watu wasiopungua 18,000 wamehamishwa kutoka katika nyumba zilizolengwa na mashambulizi ya makombora ya Iran.

Kati ya idadi hiyo ya watu, elfu 12 wamehamishiwa mahotelini na waliosalia wamepatiwa makazi katika nyumba za kupanga. 

Wachambuzi wa mambo wameeleza kuwa miji minne ikiwemo Bat Yam, Tel Aviv, Rehovot na Ramat Gan imeharibiwa pakubwa na mashambulizi ya makombora ya Iran huku uhaba mkubwa wa nyumba ukiwakumba walowezi waliokimbia makazi yao.

Tzvika Brot Meya wa mji wa Bat Yam amefichua hasara na uharibifu mkuwa uliosababishwa na mashambulizi ya makombora ya Iran dhidi ya mji huo. 

Meya huyo ameendelea kusema kuwa shambulio la siku moja la Iran limesababisha uharibifu mkubwa kuwahi kushuhudiwa katika ardhi zote zinazokaliwa kwa mabavu, si tu huko Bat Yam.

Makadirio yaliyofanywa yanaonyesha kuwa uharibifu uliosababishwa na makombora ya Iran utapelekea kupanda kwa bei za nyumba kwa muda.

Utawala haramu wa Israel ulitekeleza mashambulizi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu tarehe 13 mwezi huu wa Juni kwa kuungwa mkono na  Marekani, na kuwaua makamanda kadhaa wa ngazi za juu wa kijeshi, wanasayansi na raia wengine kadhaa wa kawaida wakiwemo wanawake na watoto. 

Siku hiyo hiyo, vikosi vya ulinzi vya Iran, vikiongozwa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) vilianzisha oparesheni kubwa ya kulipiza kisasi dhidi ya utawala wa Israel kwa jina la Ahadi ya Kweli III.