Nafasi ya Uingereza katika vita vya Gaza yamulikwa; Mashinikizo yashtadi kwa ajili ya kufanyika uchunguzi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i127946-nafasi_ya_uingereza_katika_vita_vya_gaza_yamulikwa_mashinikizo_yashtadi_kwa_ajili_ya_kufanyika_uchunguzi
Huku idadi ya Wapalestina wanaouawa shahidi ikiongezeka huko Gaza, mashinikizo ya kuitaka serikali ya Uingereza kufanya uchunguzi huru kuhusina na mchango wa nchi hiyo katika vita vya Gaza yanazidi kuongezeka.
(last modified 2025-07-05T00:46:16+00:00 )
Jul 05, 2025 00:46 UTC
  • Nafasi ya Uingereza katika vita vya Gaza yamulikwa; Mashinikizo yashtadi kwa ajili ya kufanyika uchunguzi

Huku idadi ya Wapalestina wanaouawa shahidi ikiongezeka huko Gaza, mashinikizo ya kuitaka serikali ya Uingereza kufanya uchunguzi huru kuhusina na mchango wa nchi hiyo katika vita vya Gaza yanazidi kuongezeka.

Jeremy Corbyn, kiongozi wa zamani wa chama cha Labour nchini Uingereza amesisitiza kuwa, misaada ya kijeshi na kisiasa wa London kwa utawala wa Kizayuni wa Israel ni lazima ichunguzwe kwa kina.

Corbyn, ambaye pamoja na wabunge kadhaa wanaoiunga mkono Palestina wanataka kuunda chama kipya cha siasa, amesema katika waraka alioutuma kwa gazeti la Morning Star kwamba: "Kama ilivyofichuliwa katika ripoti ya Chilcot kuhusu mapungufu ya serikali katika vita vya Iraq, uchunguzi huru kuhusu kushiriki Uingereza katika jinai za kivita za  Israel hauepukiki licha ya kuwepo ukwamishaji mkubwa. 

Mkuu huyo wa zamani wa chama cha Labour ameongeza kuwa pendekezo hili hadi sasa limeungwa mkono na zaidi ya wabunge 50 wa Uingereza na mashirika kadhaa mashuhuri ya haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na Oxfam, Action Aid na taasisi mbalimbali. 

Corbyn pia amesema tayari limeundwa "Kundi la Hague" ambalo ni muungano wa nchi tisa kwa lengo la kuratibu hatua za kisheria, kidiplomasia na kiuchumi dhidi ya ukiukaji wa sheria za kimataifa unaofanywa na utawala wa Israel. Hatua hizi ni sehemu ya mashinikizo ya kimataifa ili kuwepo uwazi na uwajibikaji.

Corbyn ametoa wito wa kufanyika uchunguzi wa wazi, kamili na huru unaohusisha maafisa wote waliohusika katika maamuzi ya kushiriki katika vita vya Israel dhidi ya Gaza tangu Oktoba 2023. Ameongeza: "Tunahitaji kujua ni silaha gani zilitumwa kwa utawala wa Israel, zipii zilitumiwa Gaza, ni ushauri gani wa kisheria ambao serikali ilipokea, na ikiwa kambi za Uingereza zilichangia au la katika kusafirisha silaha au la.