Askari wa Israel aliyekuwa vitani Ghaza na Lebanon ajiua ndani ya gari lake
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i128056-askari_wa_israel_aliyekuwa_vitani_ghaza_na_lebanon_ajiua_ndani_ya_gari_lake
Tovuti ya Kiebrania ya Walla imeripoti kuwa, mwanajeshi wa utawala wa Kizayuni Israel, Daniel Edri, amejiua kwa kujichoma moto ndani ya gari lake kwenye msitu karibu na eneo la Safed, kutokana na msongo mkali wa mawazo baada ya kuhudumu kwenye vita vya kinyama vya utawala huo dhidi ya Ghaza na Lebanon.
(last modified 2025-07-08T05:22:20+00:00 )
Jul 07, 2025 19:04 UTC
  • Askari wa Israel aliyekuwa vitani Ghaza na Lebanon ajiua ndani ya gari lake

Tovuti ya Kiebrania ya Walla imeripoti kuwa, mwanajeshi wa utawala wa Kizayuni Israel, Daniel Edri, amejiua kwa kujichoma moto ndani ya gari lake kwenye msitu karibu na eneo la Safed, kutokana na msongo mkali wa mawazo baada ya kuhudumu kwenye vita vya kinyama vya utawala huo dhidi ya Ghaza na Lebanon.

Kwa mujibu wa mama yake, Edri alikuwa mara nyingi akisafirisha miili ya wanajeshi waliouawa na akimueleza kwamba ameshuhudia maovu ya vita na kumsimulia kwa kusema: “mama, mimi ninasikia harufu ya miili na huiona kila wakati”.

Mama wa askari huyo wa kizayuni ameendelea kueleza kuwa afya ya akili ya mwanawe ilikuwa imedhoofika sana, na hivyo kumfanya atafute msaada wa matibabu. Amebainisha pia kuwa Edri alipatwa na tatizo la kupandwa na hasira ghafla kulikopelekea kufanya uharibifu mkubwa wa vitu katika nyumba yake.

Kwa mujibu wa tovuti ya Walla jeshi la Israel limekataa kumpatia askari huyo mazishi ya kijeshi, licha ya ombi lililotolewa na familia yake.

Wakati huo huo, vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni wa Israel vimeripoti kuwa idadi ya wanajeshi waliojitoa uhai tangu kuanza vita imefikia 43, kutokana na kusumbuliwa na msongo wa mawazo uliochochewa na matukio ya vita hivyo vya kinyama…/