Kwa nini shambulizi la kuvizia la Beit Hanoun ni kipigo kikubwa kwa Israel?
Wanamapambano wa harakati ya Hamas wamefanya shambulizi la kuvizia la awamu nne huko Beit Hanoun na kuua wanajeshi watano wa Israel na kuwajeruhi wengine 14.
Oparesheni ya Beit Hanoun ni kipigo kikubwa kwa Wazayuni. Katika uga wa kisiasa, operesheni hii ilitekelezwa wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, nchini Marekani na kabla ya mkutano wake na Rais wa nchi hiyo, Donald Trump. Trump na Netanyahu walitazamiwa kusherehekea madai ya ushindi wao katika vita dhidi ya mhimili wa muqawama. Oparsheni ya Beit Hanoun imeonyesha kuwa ushindi unaodaiwa na pande mbili hizo ni madai matupu, na uhakika wa mambo katika uwanja wa vita ni kinyume na madai haya.
Oparesheni ya Beit Hanoun ilikuwa na umuhimu mkubwa kwa upande wa kijeshi. Oparesheni hii imeonyesha kuwa licha ya utawala wa Kizayuni kuendeleza vita na mauaji makubwa ya kimbari kwa miezi 21, lakini muqawama wa Palestina ungali hai na unasisitiza kuendeleza mapambano dhidi ya utawala wa Israel unaoikalia Quds Tukufu kwa mabavu. Hii ni katika hali ambayo, licha ya mauaji ya kimbari yanayoendelea dhidi ya watu wa Gaza, lakini utawala wa Kizayuni umeshindwa kuvunja irada na azma ya wananchi na wanamuqawama wa Hamas.
Katika upande mwingine, oparesheni ya Beit Hanoun imedhihirisha kuwa madai yanayotolewa na Wazayuni kuhusu kuwaachilia huru wafungwa huku vita vikiendelea pia ni ya uongo. Kuhusiana na hili, harakati ya muqawama ya Hamas imesema katika taarifa yake kuwa: "Kauli mbiu za Israel za kutoa kipigo na kuiangamiza kikamilifu Hamashaziima ukweli wowote. Aidha upotoshaji wa utawala wa huo kwa ajili ya kuwaachia huru mateka kwa kutumia nguvu pia umesambaratishwa kwa vipigo mfululizo vya wapigania uhuru wa Palestina.
Nukta nyingine ni kuwa, oparesheni ya Beit Hanoun imetekelelezwa ikiwa ni muendelezo wa oparesheni za Wapalestina katika maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza ambazo zimeshika kasi katika miezi ya karibuni na zinatekelezwa karibu za kila siku katika wiki zilizopita. Juni ulikuwa mwezi mbaya zaidi kwa wanajeshi ghasibu wa Israel tangu uanzishe vita na mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza huku wanajeshi na maafisa 20 wa utawala huo wakiuawa na wengine kujeruhiwa.
Ni muhimu kuashiria nukta hii kwamba, oparesheni ya Beit Hanoun imeonyesha kuwa wanamapambano wa harakati ya Hamas wako tayari kikamilifu kijeshi kupigana vita na wanajeshi wa Kizayuni na wana uwezo wa kuushangaza utawala huo. Abu Obeida, msemaji wa Brigedi za Qassam tawi la kijeshi la Hamas amepongeza oparesheni za wanamuqawama na kueleza kuwa: Oparesheni hiyo ni kipigo kingine kwa wanajeshi wa Israel ambao walidhani kuwa walikuwa salama.
Katika upande mwingine, operesheni hiyo imeonyesha kufeli pakubwa kijeshi na pigo kwa Tel Aviv, kwa sababu shambulio hilo tata lilmefanyika katika umbali wa mita 500 kutoka uzio wa kaskazini wa Gaza. Eneo la Beit Hanoun lilikaliwa kwa mabavu na Israel tangu kuanza vita dhidi ya Gaza. Kwa sababu hiyo pia, tukio hilo limepokewa kwa hisia kali miongoni mwa wanasiasa wa Israel. Baadhi ya wanasiasa wamelitaja tukio hilo kuwa halikubaliki.
Wakati huo huo, kwa mujibu wa baadhi ya wapinzani wa serikalii ya Netanyahu, jeshi sasa linapigana huko Gaza si kwa ajili ya kuilinda Israel bali kulilinda baraza la mawaziri la muungano wenye misimamo mikali wa serikali ya Netenyahu ambapo wanajeshi wanaendelea kupoteza maisha ovyo vitani. Kwa hakika, operesheni hiyo imezidisha mizozo na mivutano ya kisiasa katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu (Israel) huku Netanyahu akizidi kukoselewa kwa malengo yake binafsi ya kuendeleza vita dhidi ya Gaza.