Nini uchambuzi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki kuhusu lengo la utawala wa Kizayuni huko Gaza?
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i128828-nini_uchambuzi_wa_waziri_wa_mambo_ya_nje_wa_uturuki_kuhusu_lengo_la_utawala_wa_kizayuni_huko_gaza
Hakan Fidan Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki ametahadharisha kuhusu nia ya utawala wa Kizayuni ya kuwaondoa wakaazi wa Gaza kutoka katika ukanda huo.
(last modified 2025-07-27T06:47:46+00:00 )
Jul 27, 2025 06:47 UTC
  • Hakan Fidan
    Hakan Fidan

Hakan Fidan Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki ametahadharisha kuhusu nia ya utawala wa Kizayuni ya kuwaondoa wakaazi wa Gaza kutoka katika ukanda huo.

Kwa mujibu wa Pars Today, Fidan amesema hayo katika mahojiano na televisheni ya NTV ya Uturuki na kueleza kwamba, "(Utawala) wa Israel unataka kulifanya kuwa tupu eneo la Ukanda wa Gaza kwa kuongeza matatizo na mateso ya watu wa ukanda huo na kuzitaka baadhi ya nchi kuzikubali."

Aliongeza: "Kwa upande mmoja, utawala wa Israel unaharibu miundombinu ya Ukanda wa Gaza, na kusababisha njaa na kuwaua wakazi wake. Kwa upande mwingine, maafisa wake wa kijasusi wanasafiri kwenda nchi nyingine kujaribu kuzishawishi kukubali kupokea idadi kubwa ya wakaazi waliokimbia makazi yao katika Ukanda wa Gaza."

Hakan Fidan

Fidan alisisitiza: "Israel inatatiza hali ya maisha katika Ukanda wa Gaza na itatekeleza mpango wake wa kuhama Ukanda wa Gaza wakati baadhi ya nchi zitatangaza utayari wao na makubaliano ya kuwapokea wakimbizi wa Kipalestina." Alisisitiza kuwa mpango huo lazima uzuiwe kutekelezwa na kuongeza: Ankara inafanya mazungumzo na nchi maalum na kuzionya kuhusu hili, lakini dunia nzima lazima iwe tayari kukabiliana na mpango huo.

Maafisa wengine wakuu wa Uturuki pia wameonya kuhusu matokeo mabaya ya vita vya Gaza na uhalifu wa Israel. Miongoni mwao ni, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alisema tarehe 22 Julai 2025 akizungumzia jinai za utawala wa Kizayuni wa Gaza kwamba: Vitendo vya Israel vinakumbusha jinai za Wanazi. Yeyote anayekaa kimya kuhusu matukio ya Gaza ni mshirika mkuu wa Israel katika uhalifu wake. Aliongeza: "Lengo letu ni kukomesha mauaji ya halaiki ambayo Israel inayafanya huko Gaza na kuhakikisha kuwa misaada inaingia katika eneo hilo."

Marekani ikiwa ni mshirika wa kimkakati wa Israel, ni mshirika wa moja kwa moja wa Tel Aviv katika kutekeleza mipango yake mibovu na isiyo ya kibinadamu dhidi ya wakaazi wa Gaza. Mwezi Februari mwaka 2025, Rais Donald Trump wa Marekani katika matamshi yanayowiana na matakwa ya utawala wa Kizayuni ya kuwatimua wakaazi wa Gaza, alitoa matamshi yenye utata ya kutaka kuondolewa kikamilifu Wapalestina wa Ukanda wa Gaza na kuwekewa maeneo mengine katika nchi jirani za Kiarabu.

Trump alikuwa amedai kuwa watu wa Gaza walikuwa wanatazamia kuondoka katika eneo hilo ikiwa mahali pazuri palikuwa pametayarishwa kwa ajili yao, na kwa maoni yake, kuna nchi ambazo zingeweza kutoa maeneo kwa ajili yao.

Mpango huo ulikabiliwa na mijibizo hasi ya kikanda na kimataifa. Muhimu zaidi, hata washirika wa Magharibi na washirika wa Marekani, kama vile Ujerumani na Ufaransa, walilaani mpango huo. Wakosoaji waliuchukulia mpango huo kuwa ni ukiukaji wa wazi wa haki za binadamu na jaribio la mauaji ya kikauumu huko Gaza.

Hata hivyo, baada ya Trump kujitoa kivitendo katika mpango wa kuwatimua wakaazi wa Gaza, utawala wa Kizayuni hivi sasa umechukua hatua wenyewe na kwa mujibu wa baadhi ya habari na ripoti, umefikia makubaliano na nchi kadhaa za Ethiopia, Indonesia na Libya kuwapa makazi wakaazi wa Gaza katika nchi hizo. Hata hivyo, utekelezaji wa mpango huo utakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa watu wa Gaza.

Kwa kuzingatia haya, sasa kuna mazungumzo ya kutekeleza mpango mwingine wa Gaza. Israel Katz Waziri wa Ulinzi wa Israel aliandaa mipango ya kuwalazimisha Wapalestina wote walioko Gaza kuhamia katika kambi za magofu ya Rafah, hatua ambayo wataalamu wa sheria na waangalizi wameitaja kuwa uhalifu dhidi ya binadamu.

Katz amesisitiza kuwa Israel inakusudia kutekeleza "mpango wa uhamiaji" na kwamba  hili litafanyika. Gazeti la Kizayuni la Haaretz limeripoti kuwa, Israel Katz ameliamuru jeshi la Israel kujiandaa kuanzisha kambi aliyoiita "mji wa kibinadamu", katika magofu ya mji wa Rafah.

Gaza

Katz alisema kuwa Wapalestina watapitia "uchunguzi wa usalama" kabla ya kuingia na hawataruhusiwa kuondoka katika mji unaoitwa wa kibinadamu mara tu watakapoingia.

Kwa mujibu wa mpango huo, awali, Wapalestina 600,000 watahamishwa katika eneo hili, na hatimaye, wakazi wote wa Gaza watakaa huko.

Waangalizi wa kimataifa wameonya kuhusu nia ya kweli ya Israel sambamba na mpango mpya wa Katz uliotangazwa wa kuanzisha "mji wa kibinadamu" huko Gaza, wakiuelezea mpango huo wa Israel kuwa unafungua njia kwa ajili ya kuwahamisha wakazi wa Gaza kwa lazima kutoka eneo hilo na kuutaja kuwa "uhalifu dhidi ya ubinadamu."