Waziri Mkuu wa Cuba alaani vita vya Gaza na kunyimwa chakula wa watu wa eneo hilo
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i129206-waziri_mkuu_wa_cuba_alaani_vita_vya_gaza_na_kunyimwa_chakula_wa_watu_wa_eneo_hilo
Waziri Mkuu wa Cuba ametuma jumbe kadhaa katika mitandao ya kijamii na kulaani sera za utawala wa Kizayuni dhidi ya wakazi wa Kipalestina wa Ukanda wa Gaza za kuzuia kutolewa bidhaa za chakula na kuwasababisha njaa wakazi wa eneo hilo.
(last modified 2026-09-03T12:21:49+00:00 )
Aug 06, 2025 03:23 UTC
  • Waziri Mkuu wa Cuba alaani vita vya Gaza na kunyimwa chakula wa watu wa eneo hilo

Waziri Mkuu wa Cuba ametuma jumbe kadhaa katika mitandao ya kijamii na kulaani sera za utawala wa Kizayuni dhidi ya wakazi wa Kipalestina wa Ukanda wa Gaza za kuzuia kutolewa bidhaa za chakula na kuwasababisha njaa wakazi wa eneo hilo.

Manuel Marrero Cruz ameatuma jumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X na kuzitaja mbinu za utawala wa Kizayuni kuwa ni mkakati unaotekelezwa kwa lengo la kuiangamiza jamii ya watu wa Gaza. 

Amesisitiza kuwa Cuba inaunga mkono na kufungamana na malengo ya Palestina na inapinga mashambulizi na mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni. " Tunaunga mkono njia ya ufumbuzi wa amani." 

Msimamo huu uliodhihirishwa na Waziri Mkuu wa Cuba unakwenda sambamba na mshikamano wa muda mrefu wa Cuba na Palestina, ambao umeonyeshwa na serikali ya Havana katika mikutano mingi ya kimataifa. 

Tangu kuanza vita na mauaji ya kimbari ya Israel  huko Gaza tarehe 7 Oktoba 2023, idadi ya Wapalestina waliouliwa shahidi katika hujuma za utawala wa Kizayuni  kimefikia 61,020 na majeruhi wakiwa 150,671.

Pia, kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina, tangu Machi 18, mwaka huu raia 9,440 wa Palestina wameuawa shahidi na wengine 37,986 wamejeruhiwa.