Iraq yaanza upigaji kura maalum wa uchaguzi wa bunge kwa wanajeshi na wakimbizi
Mchakato wa upigaji kura maalum kwa ajili ya wanajeshi na wakimbizi katika uchaguzi wa bunge la Iraq umeanza rasmi leo Jumapili katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.
Uchaguzi huu ni wa bunge la awamu ya 6 tangu kuanzishwa kwa mfumo wa sasa wa kisiasa baada ya mwaka 2003.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la IRIB, zoezi hilo limeanza mapema leo katika mji mkuu wa Baghdad na majimbo mengine ya Iraq, likivihusisha vikosi vya usalama na jeshi la taifa hilo.
Ripoti hiyo imeeleza kuwa upigaji kura huo maalum unajumuisha pia wakimbizi wa ndani katika baadhi ya mikoa ya Iraq.
Tume ya Uchaguzi ya Iraq ilitangaza Jumamosi kuwa takriban wanajeshi na maafisa wa usalama wapatao milioni 1.3 pamoja na wakimbizi zaidi ya 26,000 wanatarajiwa kushiriki katika zoezi hilo maalum la kupiga kura leo Jumapili.