Maafisa 4 wa ngazi za juu wa CIA waangamizwa kwa mashambulizi ya Iran huko Saudia
-
CIA, Saudia yalengwa
Ripoti zinasema kuwa maafisa wanne wa ngazi za juu wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) na askari 8 wa nchi hiyo wameuawa katika shambulizi la jeshi la Iran lililolenga kituo cha shirika hilo nchini Saudi Arabia.
Ripoti zinasema kuwa, maafisa hao wa CIA wameuawa katika shambulizi la karibuni zaidi la Iran kwenye kituo hicho.
Gazeti la Washington Post limeashiria shambulizi hilo na kuandika kuwa hujuma hiyo imefanyika kwenye viwanja vya ubalozi wa Marekani mjini Riyadh na kwamba ni mafanikio mahimu kwa Iran.
Hata hivyo gazeti hilo limefanya jitihada kubwa za kuficha idadi ya maafisa wa Marekani waliouawa katika hujuma hiyo.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa, awali maafisa wengine 6 wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) walikuwa tayari wameuawa katika shambulizi la majeshi ya Iran yaliyolenga makao ya shirika hilo huko Imarati.