Middle East Monitor: Vita vya Iran huenda vikawa mwisho wa kisiasa wa Netanyahu
-
Benjamin Netanyahu
Tovuti ya Middle East Minitor imeandika makala ya uchambuzi kuhusu mashambulizi ya kichokozi ya Marekani na utawala wa Kziayuni wa Israel ikisema kuwa vita ambavyo Benjamin Netanyahu amejiandaa kwa ajili yake kwa miaka mingi yumkini vikapelekea kutengwa kisiasa na kuporomoka stratejia yake.
Tovuti hiyo imeashiria hitilafu za mielekeo kati ya Washington na Tel Aviv na kuandika: Donald Trump anafadhilisha kufikia mapatano na Iran na kuepuka mapigano mapana zaidi eneo la Asia Magharibi badala ya kuingia katika vita vya muda mrefu.
Kwa mujibu wa uchambuzi wa Middle East Monitor, Trump hana nia ya kutuma majeshi ya nchi kavu ya Marekani huko Asia Magharibi au kuingia katika vita vya muda mrefu na yumkini akajiondoa katika vita vya sasa baada ya kufikiwa mapatano ya aina fulani, au kutangaza ushindi wa kisiasa; suala ambalo litaiweka Israel katika nafasi ngumu sana.
Middle East Monitor imeashiria pia uwezo mkubwa wa jeshi la Iran na kuandika: Mbali na uwezo wa kijeshi, nchi hiyo ina mnyororo wa makundi waitifaki katika eneo la Magharibi mwa Asia na uwezo mkubwa katika sekta ya ndege za kijeshi zisizo na rubani na medani za vita; mambo ambayo yanaweza kuwa na nafasi kubwa katika kuainisha hatima ya vita vya kuuchosha upande wa pili.
Uchambuzi huo unasema: Mazingira haya yanaweza kurefusha vita kwa Israel na kuisababishia hasara kubwa, mambo ambayo kwa upande wake yatazidisha mashinikizo ya kisiasa na kiuchumi ya ndani ya utawala huo.
Uchambuzi wa Middle East Monitor unamalizia kwa kusema: Suala ambalo lilitarajiwa kusajiliwa kama mafanikio ya kistratijia ya Netanyahu sasa kuna uwezekano mwishowe likawa mojawapo ya changamoto kubwa zaidi za kisaisa za kipindi chake na mwishowe kuwa mwisho wa uhai wake wa kisiasa.