Msemaji wa al Qassam asema Iran ni safu ya mbele ya kutetea Umma wa Kiislamu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i137504-msemaji_wa_al_qassam_asema_iran_ni_safu_ya_mbele_ya_kutetea_umma_wa_kiislamu
Msemaji wa tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amepongeza mashambulizi ya makombora ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya maeneo mbalimbali ya utawala ghasibu wa Israel.
(last modified 2026-03-22T06:48:14+00:00 )
Mar 22, 2026 03:48 UTC
  • Abu Obaida
    Abu Obaida

Msemaji wa tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amepongeza mashambulizi ya makombora ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya maeneo mbalimbali ya utawala ghasibu wa Israel.

Abu Obeida amesema: Kwa fakhari kubwa, tunatazama mashambulizi makubwa ya makombora yaliyofanywa usiku huu na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) yaliyolenga maeneo ya ndani kabisa katika ardhi za adui kwa kutumia mbinu mpya na kuua na kujeruhi makumi ya Wazayuni.

Msemaji wa Izzuddin Qassam ameongeza kuwa: Mashambulizi hayo ni jibu halali si kwa uchokozi wa Wazayuni-Wamarekani tu dhidi ya Iran, bali pia kwa mauaji ya kimbari yanayofanywa dhidi ya watu wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.

Abu Obaida amesema: Adui Mzayuni haelewi isipokuwa lugha ya mabavu, na hakuna njia ya kusimamisha uchokozi wake isipokuwa kumtwisha gharama na hasara kubwa; la sivyo ataendeleza uchokozi wake dhidi ya nchi za Kiarabu na Kiislamu.

Msemaji wa tawi la kijeshi la Hamas amesema: Hii leo Jamhuri ya Kiislamu inaunda safu ya mbele wa kutetea Umma wa Kiislamu, na wachokozi watafeli katika njama zao za kutaka kuvunja azma na irada ya mataifa mbalimbali.

Abu Obaida pia amewataka watu wote wa Asia Magharibi kuungana dhidi ya adui Mzayuni na kuchukua hatua za pamoja kwa ajili ya masuala muhimu hususan ukombozi wa Palestina.

Msemaji wa Izzuddin Qassam amesema hayo baada ya mashambulizi yaliyofanywa na Iran kwa mafanikio makubwa dhidi ya mji wa kusini mwa Israel wa Arad ambako Wazayuni wasiopungua 108 wameuwa au kujeruhiwa.

Baada ya mashambulizi hayo Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amesema "tumepita katika usiku mgumu sana".

Vilevile Meya wa Arad ametoa wito wa ulazima wa kuhamishwa familia 150 za Wazayuni katika kitongoji kilicholengwa kwa makombora ya Iran.