Wananchi na vyama vya kisiasa vya Uturuki vyapinga mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran
-
Waturuki wapinga mashambulizi ya US na Israel dhidi ya Iran
Uchunguzi wa maoni nchini Uturuki unaonyesha kuwa akthari ya wananchi wa nchi hiyo wanaunga mkono msimamo wa serikali yao wa kujiweka mbali na vita vilivyoanzishwa na Marekani na Israel dhidi ya Iran. Vyama mbalimbali vya siasa nchini humo pia vimelaani mashambulizi ya pande mbili hizo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
Shirika la habari la IRNA limelinukuu gazeti la Arabi 21 na kuripoti kuwa: Uchunguzi wa karibuni uliofanywa nchini Uturuki kuhusu mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran unaonyesha kuwa akthari ya wananchi wanaunga mkono msimamo wa serikali na jitihada za Ankara za kujiweka mbali na vita hivi.
Vyama vya upinzani nchini Uturuki pia vimeungana kupinga mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran na vimetaja sababu na kutoa maelezo mbalimbali kuhusu mashambulizi haya, kuyalaani na kuiunga mkono Iran.
Chama tawala cha Uadilifu na Usawa nchini Uturuki kinaamini kuwa Israel ndio iliyoanzisha moto wa vita kwa lengo la kufanikisha mipango ya kujitanua katika eneo la Magharibi mwa Asia.
Chama hicho kimesisitiza kuwa mashambulizi ya Marekani na Irael dhidi ya nchi nyingine iliyo huru ni kinyume na sheria za kimataifa.
Chama cha Uadilifu na Usawa kimetahadharisha kuhusu matokeo hasi ya kuendelea vita hivyo, madhara yake kwa eneo zima la Magharibi mwa Asia na uwezekano wa kushiriki nchi nyingine vitani.