Hizbullah yatwanga maeneo mbalimbali ya Israel katika oparesheni 11 za droni na makombora
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i138160-hizbullah_yatwanga_maeneo_mbalimbali_ya_israel_katika_oparesheni_11_za_droni_na_makombora
Harakati ya muqawama ya Hizbullah ya Lebanon imesema kuwa imefanya operesheni 11 dhidi ya maeneo mbalimbali ya Israel, kwa kutumia ndege zisizo na rubani, makombora na mizinga katika mshambulizi yake mtawalia.
(last modified 2026-05-04T10:27:02+00:00 )
May 04, 2026 10:25 UTC
  • Mwanajeshi wa Hizbullah
    Mwanajeshi wa Hizbullah

Harakati ya muqawama ya Hizbullah ya Lebanon imesema kuwa imefanya operesheni 11 dhidi ya maeneo mbalimbali ya Israel, kwa kutumia ndege zisizo na rubani, makombora na mizinga katika mshambulizi yake mtawalia.

Hizbullah imefanya oparesheni hizo 11 huku Israel ikiendelea kukiuka usitishaji vita baada ya Tehran kutaka kusitishwa mashambulizi ya Israel katika ardhi ya Lebanon kama moja ya masharti yake ya msingi katika mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Washington.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka duru ya habari ya Hizbullah, wanamuqawama wa harakati hiyo walishambulia mikusanyiko ya kijeshi ya maadui katika mji wa Naqoura mara mbili siku ya Jumapili kwa kutumia ndege zisizo na rubani.

Operesheni nyingi za harakati ya Hizbullah ya Lebanon zilijikita zaidi katika mashambulizi dhidi ya wanajeshi adui katika mji wa Bayyadah.

Wanamuwama wa Hizbullah pia walivurumisha makombora katika mikusanyiko ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel karibu na miinuko ya Salah na katika uwanja mkuu wa mji wa Qantara.

Operesheni nyingine za Hizbullah zilijumuisha mashambulio ya makombora dhidi ya wanajeshi wa Israel na kupiga sheheha ya zana zao za kijeshi katika mji wa Houla, na katika kituo kipya cha kijeshi cha Balat.