Mkuu wa Aramco: Kufungwa Lango-Bahari la Hormuz kumesababisha ‘mshtuko mkubwa kwa usambazaji wa mafuta katika historia’
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i140420-mkuu_wa_aramco_kufungwa_lango_bahari_la_hormuz_kumesababisha_mshtuko_mkubwa_kwa_usambazaji_wa_mafuta_katika_historia’
Mkurugenzi wa kampuni kubwa ya mafuta ya Saudi Arabia ya Aramco ameeleza kuwa kufungwa Lango-Bahari la Hormuz kumesababisha "mshtuko mkubwa zaidi wa usambazaji wa mafuta katika historia," na kwamba masoko ya dunia yamepoteza mapipa ya mafuta zaidi ya bilioni 2.6 tangu kuanza kutekelezwa hatua hiyo.
(last modified 2026-08-05T02:55:35+00:00 )
Aug 05, 2026 02:51 UTC
  • Mkuu wa Aramco: Kufungwa Lango-Bahari la Hormuz kumesababisha ‘mshtuko mkubwa kwa usambazaji wa mafuta katika historia’

Mkurugenzi wa kampuni kubwa ya mafuta ya Saudi Arabia ya Aramco ameeleza kuwa kufungwa Lango-Bahari la Hormuz kumesababisha "mshtuko mkubwa zaidi wa usambazaji wa mafuta katika historia," na kwamba masoko ya dunia yamepoteza mapipa ya mafuta zaidi ya bilioni 2.6 tangu kuanza kutekelezwa hatua hiyo.

Amin Nasser alisema haya jana Jumanne katika mahojiano na kituo cha habari cha Saudi Arabia cha Al Arabiya alipokuwa akiwasilisha matokeo ya utendaji wa kampuni hiyo katika kipindi cha miezi minne ya mwaka huu.

Amesema, kufungwa Lango -Bahari la Hormuz pia kumeathiri usalama wa chakula duniani.

Inafaa kuashiria hapa kuwa Iran imetenga njia rasmi maalumu kwa ajili ya usafirishaji wa baharini kupitia njia hiyo ya maji.

Hatua hiyo inafuatilia usafirishaji halali wa mizigo kwa njia ya bahari kwa kuzingatia mkataba wa maelewano uliotiwa saini kati ya Iran na Marekani mwezi Juni mwaka huu.

Mkataba huo ulitiwa saini kwa lengo la kuhitimisha mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, yaliyoanza Februari 28.

Hata hivyo, Marekani imekuwa ikifanya kila iwezalo kudhoofisha njia hiyo rasmi ya baharini kwa kujaribu kufanikisha safari za meli kupitia njia isiyo halali kando ya pwani ya Oman.

Iran imefunga Lango Bahari la Hormuz ikijibu chokohoko hizo za Marekani na inataka kusitishwa uingiliaji kati wa Washington katika usafirishaji wa baharini kwenye njia hiyo muhimu na ya kimkakati duniani.