Uturuki, Saudi Arabia na Pakistan zasaini mkataba wa pamoja wa ulinzi huku nguvu ya Marekani ikipungua
Saudi Arabia imesaini makubaliano ya pamoja ya ulinzi kati yake na Uturuki Pakistan kwa lengo la kuimarisha usalama wa pamoja na ushirikiano wa kijeshi huku nguvu za kijeshi za Marekani zikipungua katika eneo hili.
Makubaliano ya Pamoja ya Ulinzi ya Makka yalisainiwa jana na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, Mrithi wa Ufalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman, na Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif wakati wa mkutano wa pande tatu katika Kasri ya Al-Safa katika mji huo nchini Saudi Arabia.
Pande hizo tatu zimeeleza zimeeleza katika taarifa yao kuwa makubaliano hayo yanalenga kuimarisha uwezo wa pamoja wa kuzuia uchokozi wowote; huku yakibainisha kuwa shambulio la kijeshi dhidi ya mojawapo ya nchi hizo tatu litachukuliwa kuwa ni shambulio dhidi ya nchi hizo.
Taarifa hiyo imeleza kuwa makubaliano hayo yanalenga kuimarisha usalama wa pamoja wa nchi tatu yaani Saudi Arabia, Uturuki na Pakistan; na kukuza amani, usalama na utulivu katika eneo la magharibi mwa Asia na kwingineko.
Afisa wa Uturuki amesisitiza kuwa makubaliano hayo hayajaulenga upande wowote mahususi, na kwamba yako wazi kwa nchi nyingine za kanda hii.
Asia ya Magharibi imekumbwa na mivutano na hali ya mchafukoge kwa karibu miaka mitatu tangu kuanza kwa vita vya mauaji ya kimbari vilivyoanzishwa na na Israel dhidi ya Gaza mnamo Oktoba 7, 2023.
Israel imeanzisha vita vya mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza, mashambulizi dhidi ya maeneo ya kusini mwa Lebanon na kuishambulia Syria; na wakati huo huo imeshirikiana na Marekani kuanzisha vita viwili vya kichokozi dhidi ya Iran; hujuma ambayo ilikabiliwa na jibu la Iran kwa kushambuliwa vikali kambi na maeneo mbalimbali ya Marekani na Israel katika nchi mbalimbali za kanda hii.