Ansarullah: Baraza la Usalama la UN limepoteza hadhi; maazimio yake hayana thamani
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i140506-ansarullah_baraza_la_usalama_la_un_limepoteza_hadhi_maazimio_yake_hayana_thamani
Kiongozi mwandamizi wa harakati ya Ansarullah nchini Yemen amepuzilia mbali hatua ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ya kulaani mashambulizi ya makombora ya kulipiza kisasi dhidi ya Saudi Arabia na meli za kibiashara za utawala huo wa kifalme akisema kuwa chombo hicho cha kimataifa kimepoteza uhalali na hadhi yake, na maazimio yake hayana thamani yoyote.
(last modified 2026-08-17T09:53:57+00:00 )
Aug 08, 2026 12:50 UTC
  • Hizam al-Assad
    Hizam al-Assad

Kiongozi mwandamizi wa harakati ya Ansarullah nchini Yemen amepuzilia mbali hatua ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ya kulaani mashambulizi ya makombora ya kulipiza kisasi dhidi ya Saudi Arabia na meli za kibiashara za utawala huo wa kifalme akisema kuwa chombo hicho cha kimataifa kimepoteza uhalali na hadhi yake, na maazimio yake hayana thamani yoyote.

Hizam al-Assad ambaye ni mwakilishi wa Ofisi ya Kisaisa ya harakati ya Ansarullah ya Yemen amekosoa utendaji wa Baraza la Usalama la UN kuhusiana na matukio yanayojiri nchini Yemen na Ukanda wa Gaza, akisisitiza kuwa chombo hicho mara chache hutimiza wajibu wake kama mlinzi wa amani na usalama wa kimataifa, na kwamba hadhi yake ya kuaminika imepungua.

Ameongeza kuwa, Baraza la Usalama halijachukua hatua madhubuti kuhusiana na mashambulizi na mzingiro wa muda mrefu wa Saudi Arabia dhidi ya watu wa Yemen kwa muda wa miaka 12 iliyopita.

"Kivitendo Baraza la Usalama limefeli kushughulikia mgogoro wa binadamu unaozidi kuwa mbaya kila siku huko Gaza na kusimamisha mashambulizi ya kikatili na mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya eneo hilo," amesema Hizam al –Assad Afisa mwandamizi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen.

Kiongozi huyo wa Ansarullah ametamka haya baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa kulaani mashambulizi ya makombora ya jeshi la Yemen dhidi ya Saudi Arabia na meli za kibiashara za utawala huo na kulaani pia kutua ndege katika viwanja vya ndege vya Yemen.

Julai 20 mwaka huu serikali ya Sana’a ilitangaza kuiwekea Saudi Arabia mzingiro wa majini, ikieleza kuwa serikali ya Riyadh imeiwekea Yemen “mzingira onevu wa ukandamizaji” kwa karibu miaka 12, huku “ikipora rasilimali za nchi hiyo na kudumisha mzingiro kamili.”