Jerusalem Post: Israel imeshtushwa na kasi ya Iran ya kujiimarisha upya kijeshi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i140676-jerusalem_post_israel_imeshtushwa_na_kasi_ya_iran_ya_kujiimarisha_upya_kijeshi
Gazeti la kizayuni la Jerusalem Post limefichua kuwa, maafisa wa ulinzi wa Israel wameshtushwa na namna Iran ilivyojenga upya na kwa kasi uwezo wake wa kijeshi tangu baada ya mashambulizi makali ya Marekani na utawala huo wa kizayuni wakati wa kipindi cha mwanzoni mwa vita vya kichokozi vilivyoanzishwa na tawala mbili hizo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
(last modified 2026-08-15T04:03:33+00:00 )
Aug 15, 2026 03:53 UTC
  • Jerusalem Post: Israel imeshtushwa na kasi ya Iran ya kujiimarisha upya kijeshi

Gazeti la kizayuni la Jerusalem Post limefichua kuwa, maafisa wa ulinzi wa Israel wameshtushwa na namna Iran ilivyojenga upya na kwa kasi uwezo wake wa kijeshi tangu baada ya mashambulizi makali ya Marekani na utawala huo wa kizayuni wakati wa kipindi cha mwanzoni mwa vita vya kichokozi vilivyoanzishwa na tawala mbili hizo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Mapema wiki hii, mshauri mwandamizi wa Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Brigedia Jenerali Mohammad-Reza Naqdi aliiambia televisheni ya Press TV kuwa, uundaji wa makombora ya balestiki na ndege zisizo na rubani wa Iran unazidi kiwango kinachotumika; na akaongezea kwa kusema: "Hata kama vita vitadumu kwa miaka kadhaa, makombora yetu ya balestiki yataendelea kumvurumikia adui".

Katika makala liliyochapisha kwenye toleo lake la Alkhamisi, Jerusalem Post lilisema, limethibitisha kupitia duru zake, kwamba taarifa za maafisa waandamizi wa Iran kuhusu uzalishaji wa silaha uliofanywa kwa kasi nchini humo ni sahihi kabisa.

Makala ya Jerusalem Post imekumbusha kuwa, jeshi la utawala wa kizayuni IDF limekuwa likidai kwa miezi kadhaa kwamba uwezo wa kijeshi wa Iran umerudishwa miaka kadhaa nyuma baada ya vikosi vya Marekani na utawala huo kuishambulia nchi hiyo karibu mara 30,000, na kulenga zaidi ya sehemu 2,600 za maghala ya makombora na viwanda vya kijeshi wakati wa kipindi kilchopamba moto zaidi cha vita cha baina ya mwishoni mwa Februari na mapema Aprili mwaka huu.

Lakini hivi sasa jeshi la Israel na shirika la ujasusi la utawala huo Mossad zinakiri kuwa hazikutarajia kwamba Tehran itaweza kurejesha haraka sana akiba yake ya makombora ya balestiki na silaha zingine muhimu.

Kwa mujibu wa maafisa wa utawala wa kizayuni wa Israel, Wairani sio tu waliweza kuyafikia haraka maeneo yao ya makombora ya chini ya ardhi yaliyoathiriwa na mashambulizi ya anga ya Marekani na Israel, lakini pia waligundua njia zingine za ubunifu za kuunda upya silaha zao…/