Waziri Mkuu wa Pakistan: Uvamizi dhidi ya Iran ndio sababu kuu ya mgogoro wa kikanda
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i141124-waziri_mkuu_wa_pakistan_uvamizi_dhidi_ya_iran_ndio_sababu_kuu_ya_mgogoro_wa_kikanda
Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif, amesema kuwa ukiukaji wa mamlaka ya kujitawala na ardhi ya Iran mapema mwaka huu umesababisha mgogoro mkubwa wa kikanda, na kusisitiza kuwa diplomasia ndiyo njia pekee endelevu ya kutatua mgogoro huo.
(last modified 2026-09-01T14:19:31+00:00 )
Sep 01, 2026 14:17 UTC
  • Shehbaz Sharif akosoa uvamizi dhidi ya Iran
    Shehbaz Sharif akosoa uvamizi dhidi ya Iran

Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif, amesema kuwa ukiukaji wa mamlaka ya kujitawala na ardhi ya Iran mapema mwaka huu umesababisha mgogoro mkubwa wa kikanda, na kusisitiza kuwa diplomasia ndiyo njia pekee endelevu ya kutatua mgogoro huo.

Akihutubia mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) mjini Bishkek nchini Kyrgyzstan, Sharif ameweka wazi misimamo ya Pakistan kuhusu masuala ya kikanda, utekelezaji wa makubaliano ya Islamabad ya kuhitimisha vita baina ya Iran na Marekani, hali ya mambo huko Palestina, matukio ya eneo la Kusini mwa Asia na Afghanistan, pamoja na fursa za kupanua ushirikiano wa nchi mbili na wa pande kadhaa katika fremu ya Jumuiya ya Shanghai.

Waziri Mkuu wa Pakistan amesema Iran ambayo ni nchi mwanachama wa SCO mapema mwaka huu ilikabiliwa na mashambulizi, jambo lililosababisha kukiukwa mamlaka ya kujitawala nchi na umoja wa ardhi ya nchi hiyo na kuibua mgogoro mkubwa katika kanda ya Magharibi mwa Asia.

"Kuvurugika njia za usafirishaji kulikosababishwa na hali hiyo kumeathiri uchumi wa dunia na maisha ya watu, huku Pakistan na nchi nyingine nyingi zikikabiliwa na madhara kutokana na ukosefu wa utulivu eneo hili," ameeleza Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif.

Katika hotuba yake huko Bishkek nchini Kyrgyzstan, Sherif kwa mara nyingine tena amesisitiza dhamira thabiti ya Pakistan ya kudumisha amani, na kusema Islamabad itaendelea kutekeleza wajibu wa dhati katika juhudi za upatanishi na uwezeshaji zinazolenga kutatua migogoro mbalimbali.