Yemen: Shambulio la Marekani kwenye hafla ya harusi nchini Iran ni uhalifu kamili wa kivita
Taasisi ya Kitaifa ya Haki za Binadamu ya Yemen imelaani vikali uhalifu wa kivita uliofanywa na Marekani katika shambulio dhidi ya hafla ya harusi huko Sirik, kusini mwa Iran.
Katika mwendelezo wa matamko ya kulaani jinai dhidi ya ubinadamu iliyofanywa na Marekani kwa kulenga hafla ya harusi katika Wilaya ya Sirik, mkoani Hormozgan, kusini mwa Iran, Taasisi ya Kitaifa ya Haki za Binadamu ya Yemen imetoa taarifa ikisema:
“Tunalaani vikali jinai ya kikatili iliyofanywa na adui Marekani kwa kushambulia hafla ya harusi nchini Iran, shambulio ambalo limesababisha kuuawa na kujeruhiwa kwa makumi ya raia.”
Taasisi hiyo ya Yemen imeongeza kuwa shambulio hilo la kikatili ni uhalifu kamili wa kivita na ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa za kibinadamu pamoja na Mikataba minne ya Geneva; mikataba ambayo inachukulia kulenga maeneo ya kiraia na maeneo salama ya makazi kuwa ni uhalifu.
Taarifa hiyo imeendelea kusema:
“Taasisi ya Kitaifa ya Haki za Binadamu ya Yemen inalaani vikali uchokozi huu wa hiana na wa kihalifu uliofanywa na Marekani, na inaitaja serikali ya Marekani kuwa inawajibika kwa kumwaga damu ya watu wasio na hatia na kusababisha hofu na taharuki miongoni mwa raia.”
Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imeeleza: “Damu ya raia hawa wasio na hatia wa Iran haitapotea bure kamwe. Itabaki kuwa doa la aibu kwenye paji la uso la wote walioshiriki katika uchokozi huu, waliouhalalisha au kuuchukulia kwa ukimya.”
Wakati huo huo, vikosi vya ulinzi vya Iran vimetekeleza mfululizo wa operesheni kali za kulipiza kisasi ambazo zimehusisha mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani zilizolenga kambi na maslahi ya Marekani katika eneo la Asia Magharibi kufuatia vitendo vya hivi karibuni vya utawala huo wa kigaidi vya kuanzisha uchokozi usio na sababu, ambao umepelekea kuuawa shahidi raia kadhaa wasio na hatia wa Jamhuri ya Kiislamu akiwemo mtoto mdogo.