Katibu Mkuu wa Harakati ya Nujaba: Kuanzia mwezi ujao, hatutambakisha hai mwanajeshi hata mmoja wa Marekani nchini Iraq
-
Akram Al-Kaabi
Katibu Mkuu wa harakati ya al Nujaba ya Iraq amesema kwamba Kambi ya Muqawama imejitayarisha kikamilifu kwa ajili ya kuwafukuza wanajeshi wa kigeni nchini humo tarehe 30 mwezi huu wa Septemba, na kwamba baada ya tarehe hiyo, hatutamwacha hai hata mwanajeshi mmoja wa Marekani atakayesalia nchini Iraq.
Akram Al-Kaabi, Katibu Mkuu wa harakati ya mapambano ya al Nujaba ya Iraq, amesema: Donald Trump ni mjinga mwenye njozi ambaye hawezi kupata ushindi nchini Iraq, hasa baada ya kushindwa nchini Iran.
Al-Kaabi amesema: Ikiwa Iran ilimtia woga rais wa Marekani na kumfanya ajifiche kwenye kwenye jokofu na kubeba chakula, Iraq itamsababishia kiharusi hivi karibuni.
Katibu Mkuu wa harakati ya al Nujaba ya Iraq ameendelea kwa kusema: "Trump anapaswa kujua kwamba tunasubiri kwa hamu na utayarifu kamilifu Septemba 30, tarehe ya kuondoka vikosi vya majeshi ya Marekani kwenye ardhi ya Iraq, ili kama vikosi hivyo vamizi vitakengeuka ahadi yao ya kuondoka kabisa nchini Iraq, tuanzishe vita vya maamuzi dhidi ya vikosi hivyo."
Al-Kaabi amesema: "Trump ni mtaalamu wa kusema muongo na anafanya propaganda za kupata ushindi kwenye vyombo vya habari; lakini hatutamruhusu kamwe kutimiza malengo yake."
Itakumbukwa kuwa, Waziri Mkuu wa Iraq, Ali al-Zaidi ametangaza kwamba Septemba 30 itakuwa "tarehe ya mwisho wa shughuli za kijeshi ya muungano wa kimataifa dhidi ya ISIS nchini Iraq na siku ya mwisho ya vikosi vya muungano huo unaoongozwa na Marekani katika ardhi ya Iraq."