Mazishi ya Wapalestina 100 waliouliwa shahidi yafanyika Gaza; watoto 70 ni miongoni mwa mashahidi hao
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i141248-mazishi_ya_wapalestina_100_waliouliwa_shahidi_yafanyika_gaza_watoto_70_ni_miongoni_mwa_mashahidi_hao
Mazishi ya Wapalestina 100 waliouliwa shahidi yafanyika Gaza; watoto 70 ni miongoni mwa mashahidi hao
(last modified 2026-09-06T11:36:12+00:00 )
Sep 06, 2026 11:32 UTC
  • Mazishi ya mashahidi 100 wa Kipalestina Ukanda wa Gaza
    Mazishi ya mashahidi 100 wa Kipalestina Ukanda wa Gaza

Mazishi ya Wapalestina 100 waliouliwa shahidi yafanyika Gaza; watoto 70 ni miongoni mwa mashahidi hao

Idara ya Ulinzi wa Raia na Uokoaji ya Gaza imearifu kuwa miili hiyo ilipatikana hivi karibuni kutoka chini ya vifusi baada ya siku kadhaa za operesheni za utafutaji na uokoaji.

Shughuli ya mazishi ya wahanga hao, ambao miili yao imetolewa hivi karibuni kwenye vifusi, imefanyika katika mtaa wa Zeitoun, mashariki mwa Gaza.

Wizara ya Afya ya Palestina huko Gaza imesema katika taarifa yake mpya kwamba tangu kusitishwa mapigano kulipoanza kutekelezwa tarehe 11 Oktoba, watu 1,344 wameuawa na wengine 4,464 kujeruhiwa, huku miili ya wahanga 815 ikipatikana kutoka chini ya vifusi.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa idadi ya watu waliouwa katika vita na mauaji ya kimbari ya utawala ghasibu wa Israel huko Gaza tangu Oktoba3,2023 imeongezeka hadi 73,651 huku wengine 174,575 wakijeruhiwa.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, maelfu ya waathiriwa bado wamenaswa chini ya vifusi na katika mitaa mbalimbali; na hadi sasa timu za uokoaji na ulinzi wa raia zimeshindwa kuwafikia.