Tovuti ya kizayuni: Ishara za kushindwa Marekani katika vita na Iran ziko wazi kabisa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i141480-tovuti_ya_kizayuni_ishara_za_kushindwa_marekani_katika_vita_na_iran_ziko_wazi_kabisa
Tovuti moja ya habari ya Kizayuni imeandika kuwa, Marekani inajiona ndiye mshindi katika vita wakati Pentagon inakiri kwamba ina uhaba wa silaha, huku bei ya mafuta ikipanda na kufikia $110, na Mlango-Bahari wa Hormuz na ule wa Bab al-Mandab ikiwa imewekewa mzingiro kamili.
(last modified 2026-10-15T07:22:56+00:00 )
Sep 15, 2026 10:50 UTC
  • Tovuti ya kizayuni: Ishara za kushindwa Marekani katika vita na Iran ziko wazi kabisa

Tovuti moja ya habari ya Kizayuni imeandika kuwa, Marekani inajiona ndiye mshindi katika vita wakati Pentagon inakiri kwamba ina uhaba wa silaha, huku bei ya mafuta ikipanda na kufikia $110, na Mlango-Bahari wa Hormuz na ule wa Bab al-Mandab ikiwa imewekewa mzingiro kamili.

Tovuti ya Kizayuni ya "Central Issue" imeeleza katika makala iliyoandikwa na mhariri wake mkuu Rami Yizhar kuhusu "upeo wa kushindwa kimkakati Marekani katika vita vyake visivyo na ulazima dhidi ya Iran na matokeo yake ya muda mrefu."

Yizhar ameeleza katika makala hiyo: "hivi sasa, kile ambacho Rais wa Marekani Donald Trump, alijaribu kukificha kwa gharama yoyote ile, na kile ambacho waziri wake wa vita, Pete Hegseth, alikuwa akikikanusha vikali katika simulizi zake za huko nyuma, kimedhihirika wazi kwa kila mtu."

Akielezea matokeo hasi ya vita dhidi ya Iran, mhariri mkuu huyo wa tovuti ya Central Issue amesema: "Mlango-Bahari wa Hormuz umefungwa, bei ya mafuta ni karibu dola 110 kwa pipa, mfumuko wa bei unaongezeka, na akiba ya risasi za Marekani inapungua vibaya sana. Vita vipya na vikali sana ambavyo Sana'a imeanzisha dhidi ya Saudi Arabia navyo pia vinaifanya hatari ya udhibiti hatari wa Bab al-Mandab ikaribie zaidi."

Amebainisha kuwa ripoti rasmi ya kwanza ya Mkaguzi Mkuu wa Idara ya Vita ya Marekani inathibitisha jambo ambalo serikali ya Washington ilikuwa imelikanusha kwa miezi kadhaa: "Vita na Iran vimesababisha uhaba wa risasi na kuvuruga mnyororo wa usambazaji, kiasi kwamba Pentagon imelazimika kuchukua hatua za haraka za kununua silaha, kuhifadhi malighafi na vifaa muhimu, na kuharakisha shughuli za uzalishaji."

Yizhar ameongezea kwa kusema: "kwa hiyo, vita hivi vimedhihirisha kikomo halisi cha nguvu za Marekani: pesa zinaweza kuchapishwa na kukusanywa haraka, lakini makombora ya kisasa hayawezekani".

Mchambuzi huyo wa Kizayuni amebainisha pia kwamba duniani kote na hasa Marekani, kuna minong'ono inayozidi kuongezeka kwamba Benjamin Netanyahu ndiye mhusika mkuu wa kuburuzwa na kushindwa Marekani katika vita hivi…/