Larijani asisitiza kuendelea uungaji mkono wa Tehran kwa Damascus katika vita dhidi ya magaidi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i59204-larijani_asisitiza_kuendelea_uungaji_mkono_wa_tehran_kwa_damascus_katika_vita_dhidi_ya_magaidi
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesisitiza kuendelea uungaji mkono wa Tehran kwa Damascus katika vita dhidi ya magaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 17, 2020 04:15 UTC
  • Larijani asisitiza kuendelea uungaji mkono wa Tehran kwa Damascus katika vita dhidi ya magaidi

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesisitiza kuendelea uungaji mkono wa Tehran kwa Damascus katika vita dhidi ya magaidi.

Ali Larijani jana alikutana na kufanya mazungumzo huko Damascus mji mkuu wa Syria na Rais Bashar Assad wa nchi hiyo na kuongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina yakini kwamba Syria inaweza kuwafurusha magaidi katika maeneo yote ya nchi hiyo. 

Katika mazungumzo hayo Rais Bashar al Assad wa Syria pia amekosoa uungaji mkono wa baadhi ya nchi kwa makundi ya kigaidi huko Syria na kueleza kuwa magaidi wamewateka nyara raia huko Idlib kaskazini magharibi mwa nchi hiyo na kuwatumia kama ngao ya binadamu. 

Magaidi katika mji wa Idlib huko Syria 

Rais Assad ameashiria hali ya machafuko katika baadhi ya maeneo ya Syria na kusisitiza kuwa Damascus kamwe haitaruhusu kuendelea mchakato huo unaoitishia maisha ya wananchi. Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran Dakta Ali Larijani jana Jumapili aliwasili Damascus mji mkuu wa Syria kwa lengo la kufanya mazungumzo na viongozi wa ngazi ya juu wa nchi hiyo. Katika safari hiyo Spika Larijani alifuatana na ujumbe wa ngazi ya juu wa bunge. Baada ya ziara yake hiyo mjini Damascus, Spika Larijani alielekea Beirut mji mkuu wa Lebanon.