Muungano wa kijeshi wa Saudi Arabia waendeleza hujuma za kijeshi dhidi ya Yemen
Muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na utawala vamizi wa Saudi Arabia umeendelea kuyashambulia maenro mbalimbali ya Yemen.
Muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na utawala vamizi wa Saudi Arabia umeendelea kuyashambulia maenro mbalimbali ya Yemen.
Kanali ya Televisheni ya al-Masira imeripoti leo kwamba, Ijumaa ya leo kumeshuhudiwa ksa akali mashambulio sita ya anga katika mkoa wa Ma'arib. Aidha mashambulio kama hayo yameshuhudiwa katika maeneo ya mpakani yanayopakana na mkoanwa Najran wa Saudia.
Wakati huo huo imeelezwa kuwa, katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita, muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia umekiuka mara 145 usitishaji vita huko al-Hudaydah.
Saudi Arabia huku ikungwa mkono na Marekani na nchi nyingine kadhaa, Machi 25 mwaka 2015 zilianzisha hujuma na mashambulizi makubwa huko Yemen na kuiwekea nchi hiyo mzingiro wa baharini, angani na nchi kavu.
Vita hivyo vya kidhulma vya Saudia na waitifaki wake huko Yemen hadi sasa vimesababisha kuuliwa Wayemeni zaidi ya elfu 16, kujeruhiwa makumi ya maelfu na kuwa wakimbizi mamilioni ya wengine.
Aidha asasi na jumuiya mbalimbali za misaada ya kibinadamu zimetahadharisha mara chungu nzima kuhusiana na hali mbaya ya kibinadamu inayoikabili Yemen na hata uwezekano wa kutokea maafa ya kibinadamu katika nchi hiyo.