Sep 18, 2023 03:19 UTC
  • Brazil: Umoja wa Mataifa na Shirika la Biashara Duniani yazidi kupoteza itibari

Rais wa Brazil amesema kuwa Umoja wa Mataifa na Shirika la Biashara Duniani yanaendelea kupoteza itibari pole pole kadiri siku zinavyosonga mbele.

Kikao cha  viongozi wa "G77 + China" ambao ni muungano mkubwa zaidi wa nchi zinazostawi duniani ukiwa na wanachama 134, kimefanyika mjini Havana Chuba.

Washiriki wa kikao hicho ambao ni wakuu wa nchi 30 pamoja na ujumbe rasmi mbalimbali wa nchi 116, wametoa tamko lao la mwisho kwa ahadi ya kutia nguvu umoja na mshikamano wa kundi hilo na kustawisha zaidi na zaidi nafasi yake kimataifa.

Rais Lula Da Silva wa Brazil

 

Kwa mujibu wa tovuti ya Ikulu ya Brazil, Rais Lula da Silva wa nchi hiyo amesema wakati wa ufunguzi wa kikao hicho kwamba, nguvu za utawala duniani zitaendelea kutokuwa sawa na kusisitiza kuwa, Umoja wa Mataifa, mfumo wa Bretton Woods na Shirika la Biashara Duniani yanaendelea kupoteza itibari zao. Sisi hatuwezi kujikata mapande, bali tunapaswa tuwe na malengo ya pamoja ambayo yatazizingatia pia nchi zenye pato la chini na la kati na nchi dhaifu na maskini zaidi ili kuondoa wasiwasi wao.

Vikwazo vya kidhalimu vya nchi za Magharibi dhidi ya nchi nyingine, uzalishaji wa silaha za maangamizi ya umati na kuingia kasi sana uzalishaji wa vichwa vya silaha za nyuklia ni katika mambo yanayohatarisha mno usalama wa dunia na wakati huo huo kuzidi kupoteza itibari ya vyoimbo vikubwa vya kimataifa kama Umoja wa Mataifa ambavyo vinashindwa kutumia ushawishi wao kuzuia mambo hayo ambayo ni hatari kwa usalama wa dunia nzima.