Sep 24, 2023 07:56 UTC
  • Seneta Bob Menendez
    Seneta Bob Menendez

Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani amemtaka seneta wa chama cha Democratic, Bob Menendez, ajiuzulu kwa tuhuma za kupokea hongo.

Ni baada ya waendesha mashtaka wa Marekani kumshtaki Seneta Bob Menendez na mkewe kwa kupokea hongo kutoka kwa wafanyabiashara watatu wa New Jersey.

Kevin McCarthy, Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, ametoa wito wa kujiuzulu kwa Menendez baada ya ombi la wabunge wengi wa chama cha Democratic na Republican katika Bunge la Marekani la kutaka Menendez afunguliwe mashtaka.

Kevin McCarthy

Spika wa Mrepublican wa Kongresi ya Marekani amesisitiza kwamba, Menendez anapaswa kuacha kazi kutokana na kupokea rushwa.

Kiongozi wa wengi katika Seneti ya Marekani Chuck Schumer amesema Menendez atajiuzulu kwa muda kama Mwenyekiti wa Kamati ya Seneti ya Mahusiano ya Kigeni hadi kesi hiyo itakapoamuliwa.

Wataalamu wa masuala ya kisiasa wanaamini kuwa, kutuhumiwa Bob Menendez na mkewe kwa kupokea rushwa kutasababisha matatizo kwa Wademokrat katika uchaguzi wa mwaka ujao katika jitihada za kudumisha wingi wa viti vyao katika Seneti ya Marekani.