Dec 08, 2023 03:18 UTC
  • Trump: Nitakuwa

Katika matamshi yake mpya, Donald Trump, rais wa zamani wa Marekani amesema kuwa iwapo atashinda uchaguzi wa urais wa mwaka 2024, atakuwa dikteta katika siku ya kwanza ya uongozi wake na kulipiza kisasi kwa wapinzani wake wa kisiasa.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa, Donald Trump amesema atakuwa dikteta katika siku ya kwanza tu ya urais wake baada ya Wademocrati na baadhi ya Warepublican kutahadharisha kuwa Marekani itakuwa katika hatari ya kutawaliwa na dikteta iwapo Trump atashinda katika uchaguzi wa 2024. 

Trump amesema: "Nitakuwa dikteta siku ya kwanza tu", baada ya kuulizwa swali kwamba kama ataibuka mshindi katika uchaguzi wa Rais wa Marekani wa mwaka kesho na kuingia tena White House atatumia mamlaka aliyonayo kulipiza kisasi kwa mahasimu wake wa kisiasa au la. 

Trump ambaye anawania kushinda kiti cha raia na kuingia tena White House katika mchuano kati yake na mpinzake wake mkuu yaani Rais wa sasa Joe Biden, amesisitiza mara kadhaa kwamba atalipiza kisasi kwa mahasimu wake wa kisiasi iwapo atashinda katika uchaguzi huo na kushika hatamu za uongozi.

Rais Joe Biden wa Marekani 

Uchaguzi wa Rais wa Marekani umepangwa kufanyika Novemba mwaka kesho.