Dec 09, 2023 02:27 UTC
  • Facebook na Instagram zafunguliwa mashtaka kwa kuwezesha unyanyasaji wa watoto

Jimbo la New Mexico nchini Marekani limewasilisha kesi mahakamani likiituhumu Facebook na Instagram kuwa ni "eneo lenye rutuba" kwa wawindaji watoto.

Kesi hiyo mpya inakuja chini ya miezi miwili baada ya majimbo kadhaa ya Marekani kuishutumu Meta, kampuni inayomiliki Facebook na Instagram, kuwa inatengeneza faida "kutokana na maumivu ya watoto," kudhuru afya zao za akili, na kupotosha watu kuhusu usalama wa majukwaa yake.

Taarifa iliyotolewa na Mwanasheria Mkuu wa New Mexico, Raul Torrez imesema: "Uchunguzi wetu katika majukwaa ya mitandao ya kijamii ya Meta unaonyesha kuwa si maeneo salama kwa watoto, bali ni tovuti kuu za walaghai wanaotumia ponografia za watoto."

Kulingana na ripoti ya CNBC, kesi hiyo inasema kwamba "baadhi ya maudhui ya kuwanyanyasa watoto kingono" kwenye Facebook na Instagram "yamesambazwa mara kumi zaidi" kuliko yalivyosambaza na tovuti maarufu za ponografia.

Instagram na Facebook zinatumiwa kuyanyasa watoto

Kesi hiyo inasema kuwa mpango wa Meta unawalenga watoto mara tu wanapoingia kwenye majukwaa yake ya kijamii, ambapo inawaelekeza kwenye maeneo yasiyofaa.

Sehemu moja ya mashtaka hayo inasema: "Facebook na Instagram zimetayarisha maeneo mazuri kwa ajili ya wahalifu wanaolenga watoto kwa ajili ya ulanguzi wa binadamu na kusambaza picha za ngono ili kuwashawishi."

Tags