Safari ya mawaziri wa mambo ya nje wa Marekani na Uingereza nchini Ukraine
Safari ya Anthony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani akiwa na mwenzake wa Uingereza David Lemmy nchini Ukraine sio tu haitoi ujumbe mzuri kwa ajili ya kumaliza vita vya nchi hiyo na Russia, bali inatoa ishara mbaya ya kuongezeka moto wa vita hivyo.
Lengo la pande zote mbili za Magharibi katika safari hiyo limetangazwa rasmi kuwa ni kusisitiza kuendelea uungaji mkono wa Washington na London kwa Kyiv dhidi ya Russia na kuhakikisha kwamba maendeleo ya kijeshi, kiuchumi na kidemokrasia yanapatikana kwa manufaa ya Ukraine. Safari ya mawaziri wa mambo ya nje wa Marekani na Uingereza nchini Ukraine imekuja wakati nchi hiyo si tu imeshindwa kupata mafanikio yoyote yaliyotarajiwa na nchi za Magharibi katika vita na Russia, bali imezikatisha tamaa nchi za Ulaya kutokana na matokeo hasi ya vita licha ya kupewa misaada mingi ya kifedha na kijeshi na nchi za Magharibi.
Kwa hiyo kwa kufanya safari ya pamoja, Blinken na Lemy wanajaribu kuzitia moyo na kuzihimiza nchi hizo ziendelee kuipa Ukraine misaada ya kifedha na kijeshi bila kusita.
Moja ya masuala ya kijeshi yaliyoibuliwa karibuni na Ukraine ni kwamba nchi za Magharibi zinazoisaidia kijeshi na kifedha ziiruhusu nchi hiyo kutumia makombora ya masafa marefu kulenga maeneo ya Russia. Moscow imesema suala hilo linaweza kueneza vita vya Ukraine hadi Ulaya. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani, wakati wa safari yake nchini Ukraine, huenda Blinken akairuhusu kutumia makombora ya Marekani ya ATACMS kushambulia ardhi ya Russia, jambo ambalo iwapo litatimia huenda likapelekea vita vya Ukraine kuchukua sura mpya na pana zaidi.
Ingawa hadi sasa Russia imeonyesha subira kubwa na kujizuia kuchukua hatua yoyote muhimu katika kukabiliana na utumaji wa silaha za Magharibi nchini Ukraine, lakini itakuwa vigumu kudhani kwamba nchi hiyo itaendelea kuonyesha subira hiyo iwapo Marekani na nchi za Magharibi zitairuhusu Ukraine kutumia makombora ya masafa marefu kulenga maeneo ya Russia.
Hii ni katika hali ambayo Moscow inachukulia shambulio lolote la Ukraine katika maeneo ya ndani kabisa ya ardhi ya Russia kuwa ishara ya kuingia moja kwa moja na kwa pamoja nchi za Magharibi katika vita hivyo, jambo ambalo bila shaka litakuwa na matokeo hatari na yasiyotabirika.
Vyacheslav Volodin, Spika wa Bunge la Russia tayari amesema kuwa kama nchi za Magharibi zitairuhusu Ukraine kutumia sila za masafa marefu kulenga shabaha ndani ya ardhi ya Russia, basi Moscow itaichukulia Marekani na washirika wake wa Magharibi kama sehemu ya mzozo wa Ukaraine