Uchunguzi: Wanajeshi 250 wa Ukraine wako Idlib, Syria kutoa mafunzo ya kutumia ndege zisizo na rubani kwa magaidi
Ripoti zinasema kundi la wanajeshi 250 wa Ukraine liko katika mkoa wa Idlib nchini Syria kutoa mafunzo kwa magaidi, huku kukiwa na majaribio ya Ukraine na Marekani ya kuanzisha medani mpya ya mapigano dhidi ya vikosi vya jeshi la Russia katika nchi hiyo ya Kiarabu.
Habari zilizothibitishwa zinasema kwamba, idadi ya wakufunzi wa Ukraine ambao tayari wamewasili Idlib imefikia watu 250. Ripoti zinasema wanajeshi hao wamesambazwa katika vituo mbalimbali vya mafunzo katika mji wa Idlib na katika eneo la Jisir al-Shughur.
Ripoti zinasema, wakufunzi hao wa Kiukreni wamepangiwa kutoa mafunzo kwa magaidi wa kundi la Hay-at Tahrir al-Sham (HTS) kuhusu uzalishaji na uboreshaji wa ndege zisizo na rubani.
Ripoti zimesisitiza kuwa, "zaidi ya ndege 250 zisizo na rubani (UAVs) ziliwasilishwa kwa HTS huko Idlib katika mfumo wa vipuri zikiwa pamoja na bidhaa za kiraia.
Chanzo hicho kimefichua zaidi kwamba, "Waukreni na Wamarekani wanahamisha vita kutoka Ukraine hadi Syria ili kufungua uwanja mpya wa vita dhidi ya vikosi vya jeshi la Russia nchini Syria."
Shirika la habari la Sputnik pia limeashiria ripoti ya gazeti la Syria la Al Watan ambalo lilisema mkuu wa Idara ya Ujasusi ya Kijeshi ya Ukraine, Kyrylo Budanov, amekuwa akiwasiliana mara kwa mara na kiongozi wa Hay-at Tahrir al-Sham ili kuwaajiri wanamgambo kujiunga na jeshi la Ukraine.