Jibu la suali la leo; kwa nini Albanese anasema hakuna tena mistari myekundu baada ya yeye kuwekewa vikwazo na Marekani?
https://parstoday.ir/sw/news/world-i128272-jibu_la_suali_la_leo_kwa_nini_albanese_anasema_hakuna_tena_mistari_myekundu_baada_ya_yeye_kuwekewa_vikwazo_na_marekani
Francesca Albanese, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu, ametangaza kwamba uamuzi wa Marekani wa kumuwekea vikwazo unaonyesha kuwa hakuna tena mstari mwekundu wowote.
(last modified 2025-07-13T04:41:40+00:00 )
Jul 13, 2025 04:28 UTC
  • Jibu la suali la leo; kwa nini Albanese anasema hakuna tena mistari myekundu baada ya yeye kuwekewa vikwazo na Marekani?

Francesca Albanese, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu, ametangaza kwamba uamuzi wa Marekani wa kumuwekea vikwazo unaonyesha kuwa hakuna tena mstari mwekundu wowote.

Sababu ya hayo ni kwamba, utawala wa Trump umeonyesha kuwa haujali hata kidogo vipimo vya kimataifa, taasisi za kimataifa hususan Umoja wa Mataifa na majukumu waliyonayo maafisa wake akiwemo Albanese, kwa kufika hadi ya kuwawekea vikwazo na kuwapa adhabu za aina mbalimbali kwa sababu tu ya kutimiza wajibu wao.

Bi Albanese amesema, sasa anakabiliwa na hatari ya kuzuiliwa milki zake na kuwekewa mipaka ya kusafiri; na akatahadharisha kwamba, uamuzi wa Washington unaweza kuanzisha mwenendo "hatari" wa kuwalenga watetezi wa haki za binadamu duniani kote. Ripota huyo maalumu wa Umoja wa Mataifa amebainisha kwa kusema: "hakuna tena mistari myekundu, na jambo hili linatisha sana. Vikwazo hivi vinaweza kunizuia kusafiri. Jambo hili litakuwa na athari mbaya kwa watu ambao kwa kawaida huwa na mawasiliano na mimi, kwa sababu, kwa raia wa Marekani au wale wenye kadi za kijani, jambo hili litawatatiza sana."

Stephane Dujarric

 

Kabla ya hapo, Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric alitoa mjibizo kwa vikwazo vya Marekani dhidi ya Francesca Albanese kwa kusema: "kumwekea vikwazo Albanese kunaanzisha mwenendo hatari sana".

Baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio kutangaza vikwazo dhidi ya Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na hali ya Palestina, kwa kisingizio cha kuanzisha "kampeni ya vita vya kisiasa na kiuchumi" dhidi ya Marekani na utawala wa kizayuni wa Israel, mashirika kadhaa ya kutetea haki za binadamu, wanaharakati watetezi na makundi ya Kipalestina yametoa taarifa mbalimbali za kumuunga mkono Albanese. Miongoni mwa waliotoa taarifa hizo ni Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS ambayo imelaani vikwazo vya Marekani dhidi ya Francesca Albanese, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Palestina na kueleza kwamba hatua hiyo ni kielelezo cha namna Washington inavyounga mkono jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina.../