New York Times: Marekani ililipua kituo cha kuwazuilia wahamiaji wa Kiafrika Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/world-i128356-new_york_times_marekani_ililipua_kituo_cha_kuwazuilia_wahamiaji_wa_kiafrika_yemen
Gazeti la New York Times limekiri kuhusika moja kwa moja na kwa kimakusudi Marekani katika kulenga kituo cha wahamiaji wa Kiafrika katika Mkoa wa Saada mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka huu.
(last modified 2025-07-15T07:23:47+00:00 )
Jul 15, 2025 07:23 UTC
  • New York Times: Marekani ililipua kituo cha kuwazuilia wahamiaji wa Kiafrika Yemen

Gazeti la New York Times limekiri kuhusika moja kwa moja na kwa kimakusudi Marekani katika kulenga kituo cha wahamiaji wa Kiafrika katika Mkoa wa Saada mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka huu.

Katika ripoti yake, kuhusiana na Marekani kupuuza madai ya kuchunguza tukio hilo, imesema: "Mabomu yaliyotengenezwa na Marekani yaliharibu kituo cha kuwazuilia wahamiaji wa Ethiopia nchini Yemen, kuponda miili na kuwakata miguu na mikono."

Gazeti la New York Times linaeleza katika makala yake hiyo kwamba,"Kwa kuzingatia ukimya rasmi, walionusurika wanashangaa kwa nini," akibainisha kwa uwazi kwamba kupuuza Washington kwa maswali yaliyojitokeza kunaacha Jeshi la Anga la Marekani katika picha ya wazi ya mazingira ya "uhalifu kamili."

Likizungumzia matukio yaliyoandikwa na vyombo vya habari vya Yemen na mashirika ya kimataifa, gazeti hilo lilisema, "Walikimbia vita nchini Ethiopia, na kulengwa na mabomu ya Marekani huko Yemen."

Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International lilitoa taarifa mnamo Mei 19 kuhusu uhalifu huo, na kuuelezea kuwa "mbaya zaidi" tangu 2017, wakati Washington ilifanya uhalifu nchini Iraq ambao uliacha makumi ya wahasiriwa.

Kufuatia uchunguzi kuhusu uhalifu huo, kwa kuzingatia uchanganuzi wa picha za satelaiti, picha, video, na ushuhuda kutoka kwa wakimbizi na wafanyakazi wahamiaji wa Kiafrika, shirika hilo lilihitimisha kuwa "uhalifu huo lazima uchunguzwe kama ukiukaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu."