Russia: Mashambulio ya karibuni ya Israel dhidi ya Syria yanastahili kulaaniwa 'vikali'
https://parstoday.ir/sw/news/world-i128440-russia_mashambulio_ya_karibuni_ya_israel_dhidi_ya_syria_yanastahili_kulaaniwa_'vikali'
Russia imesema, mashambulio ya karibuni yaliyofanywa na utawala wa kizayuni wa Israel dhidi ya Syria yanastahili kulaaniwa "vikali".
(last modified 2025-07-17T10:18:18+00:00 )
Jul 17, 2025 09:57 UTC
  • Russia: Mashambulio ya karibuni ya Israel dhidi ya Syria yanastahili kulaaniwa 'vikali'

Russia imesema, mashambulio ya karibuni yaliyofanywa na utawala wa kizayuni wa Israel dhidi ya Syria yanastahili kulaaniwa "vikali".

Taarifa iliyotolewa leo na Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imesema: "mashambulizi haya, ambayo yanajumuisha ukiukaji mkubwa wa uhuru wa nchi na sheria ya kimataifa, yanastahili kulaaniwa vikali".

Huku ikiielezea mivutano ya karibuni iliyozuka nchini Syria kuwa ni ya 'kutia wasiwasi mkubwa sana' taarifa hiyo imesema, Moscow inatumai utekelezwaji wa hatua za kupunguza hali hiyo utasaidia kupunguza mvutano na kuleta utulivu nchini humo.

Aidha, taarifa hiyo imesema Russia inaamini kuwa njia ya kusuluhisha mivutano hiyo ni kupitia mazungumzo na "kuimarisha mwafaka wa kitaifa, kuheshimu haki za wawakilishi wote na jamii za makundi mseto ya watu wa Syria."

Wizara ya mambo ya nje ya Russia imeongeza kuwa, Moscow inatilia mkazo msimamo wake thabiti kuhusiana na haja ya kuheshimiwa uhuru, umoja na ardhi yote ya Jamhuri ya Kiarabu ya Syria.

Siku ya Jumatano, jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel lilianzisha mashambulizi ya anga dhidi ya mji mkuu wa Syria Damascus, pamoja na miji ya Suwayda na Daraa, kwa kisingizio cha kuilinda jamii ya Wadruze.

Shambulio jengine la anga liliripotiwa kufanywa na jeshi la kizayuni mapema leo Alkhamisi kwenye kituo kimoja cha jeshi cha Syria.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Syria imesema mashambulizi hayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 30 na kujeruhi wengine karibu 100.../