Jibu la suali la leo; nini sababu ya waziri wa zamani wa mambo ya nje wa US kukosoa sera ya Trump kuhusiana na Iran?
https://parstoday.ir/sw/news/world-i128468-jibu_la_suali_la_leo_nini_sababu_ya_waziri_wa_zamani_wa_mambo_ya_nje_wa_us_kukosoa_sera_ya_trump_kuhusiana_na_iran
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Anthony Blinken, amekosoa mwelekeo wa rais wa nchi hiyo Donald Trump kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran; na licha ya kuibua madai mengine mapya amesema: Iran bado haijaamua kuunda silaha za nyuklia na imetekeleza ahadi zake katika JCPOA.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Jul 18, 2025 08:53 UTC
  • Jibu la suali la leo; nini sababu ya waziri wa zamani wa mambo ya nje wa US kukosoa sera ya Trump kuhusiana na Iran?

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Anthony Blinken, amekosoa mwelekeo wa rais wa nchi hiyo Donald Trump kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran; na licha ya kuibua madai mengine mapya amesema: Iran bado haijaamua kuunda silaha za nyuklia na imetekeleza ahadi zake katika JCPOA.

Blinken amesema: “kwa mujibu wa JCPOA, kama Iran ingetaka kufuatilia chaguo la kuunda silaha za nyuklia, ingehitaji kwa uchache muda wa mwaka mmoja kuzalisha nyenzo za nyuklia zinazohitajika. Hii ni katika hali ambayo, Trump aliyachana makubaliano ya JCPOA na wala hakuyatafutia makubaliano mengine mbadala; na hatua yake hiyo imekuwa sababu ya kuongezeka kasi ya mpango wa nyuklia wa Iran”.

Waziri huyo wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani amekiri kwa kusema: haijalishi wengine watasemaje, lakini Iran iliheshimu makubaliano ya JCPOA, na baada ya Trump kujitoa katika mapatano hayo, ilijitokeza hali mbaya sana ya kutoaminiana. Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki na vilevile wataalamu wa intelijensia wa Marekani walitangaza kuwa Iran iliheshimu JCPOA. Baada ya Trump kujitoa katika JCPOA, ilikuwa vigumu mno kufanya mazungumzo ya aina yoyote na Wairani, na kulikuwa na hofu kubwa kwamba makubaliano hayo mapya yangevunjwa tena na Trump.

Trump

 

Katika ungamo lake jipya, Blinken amebainisha kwamba: alikuwa ni Obama ambaye alitayarisha silaha zilizohitajika kwa ajili ya kuishambulia Iran, ikiwa ni pamoja na mabomu mazito ya kuvunja vigingi vya chini ya ardhi. Naye Biden akaukamilisha mpango huo wakati wa urais wake. Blinken ameongeza kuwa: lakini kulingana na uchambuzi uliofanywa na serikali zote za Marekani isipokuwa ya Trump, hatua yoyote ya kijeshi dhidi ya Iran huenda itaweza kuchelewesha mpango wake wa nyuklia kwa miaka miwili au chini ya hapo, na katika kipindi hicho, Iran inaweza kuuhamishia mpango wake wa nyuklia chini zaidi ya ardhi na kuuendeleza kwa kasi kubwa.

Blinken ametahadharisha kwa kusema: "Iwapo Trump hatafikia makubaliano mapya na Iran, tutakuwa katika mazingira mabaya zaidi. Iran inaweza kujenga vituo vyake katika maeneo yanayoweza kuhimili mabomu mazito ya kuvunja vigingi vya chini ya ardhi". Kuhusiana na hila unayotaka kufanya utawala wa Kizayuni ya kutumia kigezo cha Libya kwa ajili ya Iran, Blinken amesema: "matukio ya Libya yangali yamo kwenye vichwa vya watu wengi, ikiwemo Iran. Iran haitakubali kamwe kuridhia jambo kama hilo"…/