Kuipachika Venezuela lebo ya ugaidi; shutuma za kisiasa au kisingizio cha shambulio?
https://parstoday.ir/sw/news/world-i134496-kuipachika_venezuela_lebo_ya_ugaidi_shutuma_za_kisiasa_au_kisingizio_cha_shambulio
Katika hatua yake ya hivi karibuni dhidi ya serikali ya Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, Rais wa Marekani Donald Trump ameitangaza serikali hiyo kuwa ni ya kigaidi na ameamuru kuzuiwa meli zote za mafuta zinazoingia au kutoka nchini humo.
(last modified 2025-12-20T02:23:59+00:00 )
Dec 20, 2025 02:23 UTC
  • Kuipachika Venezuela lebo ya ugaidi; shutuma za kisiasa au kisingizio cha shambulio?
    Kuipachika Venezuela lebo ya ugaidi; shutuma za kisiasa au kisingizio cha shambulio?

Katika hatua yake ya hivi karibuni dhidi ya serikali ya Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, Rais wa Marekani Donald Trump ameitangaza serikali hiyo kuwa ni ya kigaidi na ameamuru kuzuiwa meli zote za mafuta zinazoingia au kutoka nchini humo.

Kulingana na Pars Today, Rais wa Marekani alidai kwenye mtandao wake wa kijamii wa"Truth Social" kwamba Venezuela imezingirwa kabisa na kundi kubwa zaidi la meli za kivita kuwahi kukusanywa katika historia ya Amerika Kusini. ​​Kundi hili la meli litakuwa kubwa zaidi na mshtuko wao hautaweza kulinganishwa na chochote walichowahi kuona, mpaka watakaporejesha Marekani mafuta yote, ardhi na mali nyingine zote walizotunyang'anya hapo awali.

Katika hali ambayo, uwezekano wa vita vya Marekani dhidi ya Venezuela umeongezeka ambapo Marekani, bila ushahidi wowote, Novemba 24 mwakka huu ilitangaza "Cartel de Los Solis", kundi linalodaiwa kuwa shirika la kigaidi la kigeni, na kuweka vikwazo dhidi yake. Marekani ilidai kuwa Rais wa Venezuela na maafisa kadhaa waandamizi wa nchi hiyo wanaongoza kundi hilo na kupitia kwalo dawa za kulevya huingizwa nchini Marekani. ​​Madai ya Washington yanakuja wakati Venezuela ilitangaza kuwepo kwa kundi hilo kama "uwongo wa kichekesho" na kisingizio cha kuingilia kati kinyume cha sheria katika mambo yake ya ndani.

Kufuatia tuhuma hizo, Rais wa Marekani alituma makumi ya manowari na wanajeshi wake kwenye maji ya Karibi, na kuzingira maji ya pwani ya Venezuela. ​Hata hivyo, maafisa wa Venezuela wamekanusha mara kwa mara madai hayo ya dawa za kulevya. Rais Nicolas ​Maduro alisema: Trump, kwa kudai kuendesha "vita dhidi ya dawa za kulevya", ameifanya nchi hiyo ya Amerika Kusini kuukkabiliwa na "tishio kubwa zaidi la bara la karne". ​Hata hivyo, Trump pia ametangaza hivi karibuni uwezekano wa kushambulia Venezuela kwa nji ya nchi kavu.

Sambamba na kushadidi mvutano kati ya Washington na Caracas na uvumi wa uvamizi wa kijeshi wa Marekani nchini Venezuela, vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti kuwa karibu theluthi moja ya meli za jeshi la majini la Marekani zimewekwa katika eneo hilo na ndege za kivita zinazunguka anga ya kimataifa karibu na Venezuela.

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela

 

Mivutano kati ya Washington na Caracas imeongezeka, na uwezekano wa vita vya ardhini umeongezeka, na hatua za Trump dhidi ya Venezuela ni mojawapo ya mifano dhahiri ya sera za kuingilia kati na za kibeberu za Marekani. ​​Hatua hii sio tu ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa na msingi wa mamlaka ya kitaifa ya nchi, lakini pia inaonyesha mwendelezo wa sera ya muda mrefu ya Washington ya kutawala na kudhibiti rasilimali muhimu za nchi huru, hususan  katika eneo la Amerika ya Kusini.

Ingawa Venezuela daima imekuwa ikikodolewa kwa macho ya tamaa na Marekani kwa sababu ya kuwa na akiba kubwa zaidi ya mafuta duniani, lakini katika miaka ya hivi karibuni, na mabadiliko ya kisiasa katika uwanja wa kimataifa, vita vya Ukraine na Russia, na mabadiliko katika usambazaji wa nishati, haswa sera na matakwa ya Trump, ambayo yanalenga kufufua dikrii ya Monroe na kurejea kwa udhibiti wa Marekani kwa Venezuela, sasa suala hili limechukua wigo mpana zaidi, na udhibiti wa Venezuela na matumizi ya rasilimali zake za mafuta sasa ni muhimu zaidi kwa  Marekani. Kama Maria Elvira Salazar, mwakilishi wa Republican wa Florida, alivyokiri kuhusiana na suala hili: "Mafuta ya Venezuela ni lengo kuu la kiuchumi nyuma ya hatua za uhasama za Washington na uwekaji wa kijeshi katika eneo la Karibi." ​​Mbunge huyo wa Marekani alisema: Kwa kampuni za mafuta za Marekani, Venezuela itakuwa fursa ya dhahabu kwa sababu inamaanisha zaidi ya dola trilioni moja ya shughuli za kiuchumi.

 

Katika mkondo huu, kimsingi hatua za Marekani ni jaribio la kukata mshipa muhimu wa uchumi wa Venezuela na kuilazimisha serikali ya Maduro kusalimuu amri mbele ya matakwa ya Washington, kwani sera hii inaweza kuwa ni mwendelezo wa njia ile ile iliyoonekana nchini Iraq; ambayo ilikabiliwa na mashambulizi ya moja kwa moja na uingiliaji kati kwa sababu ya rasilimali kubwa za nishati na muqawama dhidi ya utawala wa Marekani.

Inaonekana kuwa, kutangazwa serikali ya Maduro kama "shirika la kigaidi" ni sehemu ya sera ya propaganda na upachikaji lebo wa Marekani. Ukweli wa mambo ni kuwa, Marekani inatumia dhana ya "ugaidi" kama chombo cha kisiasa cha kuhalalisha hatua zake za kukabiliana na mataifa yanayoipinga Marekani na matumiz ya zana za kijeshi na kiuchumi na vitendo vya kupindua serikali zinazopingana na Washington ni mfano wazi wa ugaidi.

Tajiriba ya historia inaonyesha kuwa, mataifa yanapinga sera za kibeberu. ​​Venezuela pia imeendelea kusimama dhidi ya shinikizo la Marekani kwa kutegemea msaada wa umma na mshikamano wa kikanda. ​​Kile kinachotokea Venezuela leo ni mfano wazi wa mgongano kati ya madai ya Marekani kuhusu amani na demokrasia na ukweli wa sera zake za kijeuri na za kibeberu; mgongano ambao unazidi kuwa wazi kila siku na unatia shaka uhalali wa madai ya Washington duniani kote.