Zilzala ya kisiasa yatishia Kombe la Dunia 2026... Ujerumani yadokeza kususia au kufutwa mashindano hayo
-
Trump na Giovanni Infantino
Mashindano ya Kombe la Dunia 2026, yaliyopangwa kufanyika msimu ujao wa joto Amerika Kaskazini, yanakabiliwa na tishio lisilo la kawaida, baada ya sauti nyingi nchini Ujerumani kuibuka zikitaka kususiwa Kombe la Dunia la mpira wa miguu," na hata kutoa wito wa kufutwa kabisa mashindano hayo ili kupinga sera za Rais wa Marekani, Donald Trump.
Katika taarifa muhimu kwa France-Presse, Waziri wa Nchi wa Michezo wa Ujerumani, Christiane Schneiderlein amethibitisha kwamba Serikali ya Shirikisho haitaingilia moja kwa moja uamuzi wa kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia FIFA 2026 au la, akisema: "Kazi ya tathmini iko mikononi mwa Chama cha Soka cha Ujerumani na FIFA, na serikali itakubali kile ambacho vyombo hivyo vitaamua."
Schunderlein, ambaye ni mwanachama wa chama cha Kansela Friedrich Merz, ameongeza kwamba Berlin inaheshimu "uhuru wa michezo," lakini imeacha mlango wazi kwa mashirikisho kuchukua msimamo thabiti wa kukabiliana na Marekani.
Mgogoro huu si kuhusu mpira wa miguu pekee, bali una mizizi mirefu ya kisiasa na kiuchumi, ambayo inaweza kufupishwa katika mambo mawili, yaani mgogoro wa Greenland, ikiwa na maana ya nia ya Donald Trump ya kunyakua kisiwa hicho, ambacho ni sehemu ya utawala wa Denmark, na
vita vya kibiashara hasa tishio la Washington la kutoza ushuru mkubwa kwa nchi za Ulaya zinazopinga sera zake.
Mbunge Roderich Kiesewetter wa Ujerumani pia amesema waziwazi kwamba: "Iwapo Trump atatekeleza vitisho vyake, itakuwa vigumu kuona nchi za Ulaya zikishiriki kwenye mashindano ya Kombe la Dunia," huku Mbunge Jürgen Hardt akienda mbali zaidi na kusema kwamba, mashindano hayo "yafutwe" kama njia ya mwisho ya kumrudisha rais wa Marekani kwenye akili zake.
Wakati huo huo, kura ya maoni ya hivi karibuni iliyofanywa na Taasisi ya INSA imefichua matokeo ya kushangaza; 47% ya Wajerumani wameunga mkono wazo la kususia Kombe la Dunia FIFA 2026 iwapo Washington intanyakua eneo la Greenland, ikilinganishwa na 35% waliopinga wazo hilo.
Marekani ni mwenyeji wa mashindano ya mwaka huu ya Kombe la Dunia ikishirikiana na nchi za Canada na Mexico. Marekani itakuwa mwenyeji wa mechi 78 kati ya 104 za mashindano hayo.