Nara za “Mauti kwa Marekani” zatanda kwenye anga ya barabara za Rome na Vienna
Mamia ya wanachama wa asasi zinazopinga vita, wanaharakati wa haki za binadamu na wapinzani wa uchokozi wa kijeshi wa Marekani na utawala wa kizayuni dhidi ya Iran wameandamana katika mitaa na barabara kuu za miji ya Rome, Italia na Vienna, Austria huku wakipiga nara na kaulimbiu za “Mauti kwa Marekani”.
Huku wakiwa wamebeba bendera za Iran, mabango na maberamu yaliyoandikwa nara za malalamiko, waandamanaji mjini Rome wametangaza upinzani wao dhidi ya kuendelezwa uchokozi wa kijeshi na madhara yake kwa raia.
Washiriki wa maandamano hayo wamepiga nara dhidi ya sera za kushupalia vita za Washington na kutilia mkazo ulazima wa kusitishwa vita mara moja na kurejea kwenye mkondo wa diplomasia.
Mjini Vienna, Austria waandamanaji waliokusanyika kwenye mzunguko wa Stephans Platz wametoa kaulimbiu za “Mauti kwa Marekani” na “Mauti kwa Israel” na kulaani uchokozi wa kijeshi walioanzisha hivi karibuni dhidi ya Iran.
Katika nara na kaulimbiu zao, waandamanaji hao wamelaani pia kuuliwa shahidi Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu na raia wa kawaida katika mashambulio ya karibuni ya Marekani na utawala wa kizayuni na kutilia mkazo ulazima wa kuwajibishwa wahusika wa jinai hizo kulingana na misingi ya sheria za kimataifa…/