Afisa wa zamani wa Pentagon: Hatukudhani makombora ya Iran yatakuwa ya kisasa kiasi hiki
-
Makombora ya Khaybar ya Iran yakielekea Israel
Mshauri wa zamani wa Wizara ya Vita ya Marekani (Pentagon) amekiri kuhusu uwezo mkubwa wa makombora ya Iran na udhaifu wa mifumo ya ulinzi wa anga ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Douglas McGregory amekiri kuwa maendeleo ya teknolojia ya makombora ya Iran hayatasawariki na ni makubwa sana kuliko ilivyokuwa ikidhaniwa na Marekani. "Makombora ya Iran yanavuka matabaka kadhaa ya mifumo ya ulinzi wa anga ya kisasa ya Marekani na Israel", ameongeza McGregory.
Amesema mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel wa Iron Dome haufanyi kazi vizuri. Amesema "licha ya kuwa Marekani inafanya juhudi za kulinda mifumo ya anga ya Israel kwa kurusha makombora lakini inaonekana kuwa Wairani wameendelea na kupiga hatua kubwa katika teknolojia ya makombora kuliko tulivyokuwa tukidhani.'
McGregory amesema: Wairani wana uwezo wa kutushughulisha kwa kutumia vichwa bandia vya makombora kisha wanarusha makombora halisi na hatari zaidi yanayopenya na kuvuka mifumo yetu ya ulinzi wa nga. Amesema kazi ya kuzuia makombora ya Iran haifai kabisa.
Ameongeza kuwa: "Kama ilivyo kawaida, vyombo vya habari vya Marekani vinasifia mafanikio ya kijeshi ya Marekani na Israel; hata hivyo naamini kwamba walimwengu hawaaamini ripoti hizo."