Vyombo vya habari vya Algeria: Kesi ya Epstein ndiyo chanzo cha moja kwa moja cha vita vya Trump dhidi ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i137234-vyombo_vya_habari_vya_algeria_kesi_ya_epstein_ndiyo_chanzo_cha_moja_kwa_moja_cha_vita_vya_trump_dhidi_ya_iran
Gazeti la Algeria "Al-Shorouk" limeandika kuwa kashfa iliyotokana na kesi ya bilionea mashuhuri na mhaifu wa ngono wa Marekani, Jeffrey Epstein, na kuhusika Rais Donald Trump katika kashfa hiyo ndiyo sababu ya moja kwa moja ya kuanzisha vita dhidi ya Iran ili kupotosha maoni ya umma nchini Marekani na duniani.
(last modified 2026-03-08T08:04:09+00:00 )
Mar 08, 2026 08:04 UTC
  • Trump akiwa pamoja na mshirika wake, Epstein
    Trump akiwa pamoja na mshirika wake, Epstein

Gazeti la Algeria "Al-Shorouk" limeandika kuwa kashfa iliyotokana na kesi ya bilionea mashuhuri na mhaifu wa ngono wa Marekani, Jeffrey Epstein, na kuhusika Rais Donald Trump katika kashfa hiyo ndiyo sababu ya moja kwa moja ya kuanzisha vita dhidi ya Iran ili kupotosha maoni ya umma nchini Marekani na duniani.

Gazeti la Al-Shorouk katika makala iliyoandikwa na "Bilal Abu Hilalah" limejadili hati za kashfa ya Epstein na uhusiano wake na vita wa Trump katika eneo Asia Magharibi na kuandika: Hivi majuzi gazeti la Daily Telegraph la Uingereza ilichapisha sehemu ya nyaraka za kesi ya Epstein, ambazo zinatoa maelezo ya kashfa ya ngono ya Trump katika kesi hiyo.

Kuchapishwa kwa maelezo hayo kunathibitisha nadharia ya André Carson, mjumbe wa Kamati ya Ujasusi ya Baraza la Wawakilishi la Marekani, ambaye amesema kwamba sababu kuu ya vita dhidi ya Iran ni jitihada za kuficha kashfa hiyo.

Kwa mujibu wa Carson, faili la Epstein ndiyo sababu ya vita vya Trump dhidi ya Iran. Mwakilishi huyo wa chama cha Democratic katika Kongresi ya Marekani amesema: "Kulikuwa na sababu moja kuu iliyomfanya Trump aanzishe vita dhidi ya Iran. Shambulio hili lilikuwa jitihada za kupotosha mazingatio ya umma kutoka kwenye kesi ya Epstein."

Makala ya Daily Telegraph, iliyochapishwa Machi 6, 2026 iliweka wazi faili la "unyanyasaji wa kingono" wa Donald Trump katika nyaraka za kesi ya Epstein.

Faili hilo lilifichua maelezo ya unyanyasaji wa kingono wa Trump dhidi ya wanawake na wasichana, wakiwemo wasichana wenye umri wa miaka 13 hadi 15.

Kesi ya ufisadi na ufuska ya Jeffrey Epstein, mfanyabiashara Myahudi, mhalifu wa ngono na mtakasaji pesa wa Marekani, imegubika fikra za umma na siasa za Marekani kwa miaka mingi na imekuwa uwanja wa vita vya kisiasa kati ya vyama vya siasa vya Marekani.